BOKO HARAMU KUWAUZA WASICHANA WALIOTEKWA

Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau Kundi la wapiganaji wa kiislamu nchini Nigeria la Boko Haram limesema linapanga kuwauza was...

Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau

Kundi la wapiganaji wa kiislamu nchini Nigeria la Boko Haram limesema linapanga kuwauza wasichana zaidi ya miambili ambao liliwateka nyara wiki tatu zilizopita.

Hii ni baada ya kundi hilo hatimaye kukiri ndilo lililowateka wasichana hao baada ya kimya cha wiki tatu tangu kutekwa nyara kwao.

Kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau alituma kanda ya video ambapo alikiri kwa mara ya kwanza kuwa kundi hilo ndilo liliwateka nyara wasichana hao.

Wasichana hao walitekwa kutoka shule moja iliyo kaskazini mashariki mwa nchi walipokuwa wajinadaa kwa mitihani yao.

Wakati huo huo mwanamke ambaye ni kiongozi wa maandamano ya kushinikiza serikali kuharakisha juhudi zake za kuwaokoa wasichana hao, nchini humo Naomi Mutah aliyekuwa amezuiliwa na polisi kwa amri ya mke wa rais wa nchi hiyo Patience Jonathan ameachiwa huru.

Kumekuwa na shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kwamba haijafanya juhudi kubwa kuwaokoa wasichana hao.

Akizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo rais wa Nigeria Goodluk Jonathan amesema kuwa atafanya awezalo kuwakoa wasichana hao.

Takriban watu 1500 wameuawa na kundi hilo mwaka huu likisema kuwa linapigana dhidi ya kile linachosema ni elimu ya kimagharabi.

Related

MNUNUZI WA NYUMBA/KIWANJA HII NI NAMNA YA KITAALAM YA KUJUA ENEO UNALONUNUA KAMA LINA MGOGORO AU HAPANA

  Na   Bashir   Yakub Makala zilizopita  nilieleza   mambo au taarifa muhimu  zinazopaswa kuwa kwenye  mkataba wako  unapokuwa unanunua  nyumba/k...

JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA VINAVYOENDEKEZA MIGOGORO

 Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi. Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa. Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi h...

MAGARI YA ABIRIA NA WATALII KUTOKA TANZANIA YARUHUSIWA KENYA

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, LAZARO NYARANDU   WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema serikali ya Kenya imekubali kuyaruhusu magari ya abiria na watalii kutoka Tanzania...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904758
item