HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MHE. DKT. SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA (MB)

HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MHE. DKT. SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO N...



HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MHE. DKT. SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015


 
UTANGULIZI. 

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Huduma za Jamii iliyochambua na kujadili makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 2014/15.

2. Mheshimiwa Spika. , napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunijalia afya njema na  kuniwezesha kutimiza majukumu yangu kama Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru wasaidizi wangu wakuu katika kusimamia elimu nchini walioteuliwa hivi karibuni na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Naibu Waziri Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama (Mbunge wa Peramiho); Katibu Mkuu - Profesa Sifuni Ernest Mchome na Naibu Katibu Mkuu Bibi Consolata Philipo Mgimba. Vile vile, napenda kuwapongeza na kuwashukuru kwa ushirikiano mzuri - Kamishna wa Elimu, Profesa Eustella Peter Bhalalusesa; Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za elimu zilizo chini ya Wizara yangu kwa ushirikiano wao wa karibu katika kuandaa bajeti hii. Aidha, napenda kuwashukuru Wahadhiri, Wakufunzi, Walimu na Watumishi wengine pamoja na Wanafunzi wote kwa kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Napenda pia kuwashukuru Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi na Vyama vya Wanataaluma, Wanafunzi na  Washirika wa Maendeleo, kwa ushirikiano wao katika kuiendeleza Sekta ya Elimu. Ninawashukuru pia wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla kwa jinsi ambavyo wameendelea kushirikiana na sekta ya elimu katika kuendelea kuimarisha elimu na mafunzo nchini. Ni matumaini yangu kuwa wizara itaendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu ili kuwezesha elimu na mafunzo yanayotolewa nchini kuendelea kuimarika na kufikia ubora ambao unahitaji kwa maendeleo ya taifa. 
 
Soma hotuba hii  icon HOTUBA YA BAJETI 2014-2015_WEMU (1.49 MB)

Related

2014/15 Government of Czech Republic Scholarships for Developing Countries’ Students

Czech Government Scholarships for Developing Countries’ Students in the field of Economics, Agriculture, Informatics, Environment and Energetic at public universities in the Czech Republic. Sch...

Reserve Bank of New Zealand Scholarships for International Students, 2014

The Reserve Bank of New Zealand offers scholarships for international students in 2014. Scholarships are available for Honours, Master’s or Final Year of PhD students in the field of Economics, F...

2014/15 UNIL Master’s Grants for International Students in Switzerland; Deadline 15th December, 2013

University of Lausanne is offering master’s grants to learn any of the courses except the Master of Medicine, Master of Arts in Public Management and Policy, Master of Arts in Sciences and Practi...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item