MTOTO ALIYEFUNGIWA NDANI MIEZI TISA KWA ULEMAVU WA MDOMO SUNGURA ATIBIWA

  Mtoto Selemani Kolineli Mushi(Miezi kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Baada ya kufanyiwa ...

 Mtoto Selemani Kolineli Mushi(Miezi kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Baada ya kufanyiwa upasuaji wa mdomo sungura
 Yohana Kolineli  mama mzazi wa mtoto huyo akiongea na mwandishi wetu ambae hayupo pichani
 Baba mzazi Kolinel Mushin kushoto akimsikiliza mkewe kwa makini baada ya mama huyo kufika kijijini kwao
Mtoto Selemani Kolineli Mushi(Miezi kumi) Kabla ya kufanyiwa upasuaji

MBEYA
Mtoto Selemani Kolineli Mushin(Miezi kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya amerejea salama Kijijini baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na kuzaliwa na matatizo ya mdomo sungura.

Mtoto huyo alifichwa ndani baada ya kuzaliwa na kutakiwa kurudi Hospitali ya Wilaya ya Chunya miezi sita baadaye lakini Baba Mzazi wa mtoto huyo aitwae Kolineli Mushin akikataa kumpeleka Hospitali akidai huo ni mpango wa Mungu.

Mwanzoni mwa mwezi Mei baada ya mtoto huyo kukutwa na mwandishi wa Mbeya yetu na kuwashauri wazazi wa mtoto ndipo walipokubali kumpeleka Hospitali ambapo dhamana hiyo ilichukuliwa na Afisa Ustawi wa jamii Anna Geleta la kusafirishwa hadi Hospitali ya CCBRT.

Selemani baada ya kupokelewa katika Hospitali ya CCBRT alifanyiwa upasuaji na kurekebishwa mdomo ambao ulikuwa ukimpa shida wakati wa kula na kupumua kwa shida na aliruhusiwa kutoka Hospitali Mei 15 Mwaka huu na kurejea Mbeya Mei 17 ambapo gharama za safari ya kwenda na kurudi na matibabu kugharamiwa na CCBRT.

Kwa upande wake Baba mzazi Kolinel Mushin na Mkewe Yohana Kolineli wameishukuru Mbeya yetu blog,  Serikali na Asasi ya CCBRT kwa kufanikisha matibabu ya mtoto wao ambapo wao walidhani kuwa ugonjwa huo usingetibika.

Aidha walimshukuru msamaria mwema Osward Mwailomo aliyetoa taarifa kwa mwanahabari na Mwenyekiti wa Kijiji cha Igundu kwa ushirikiano wake hata kufanikisha upasuaji wa mtoto na hali yake inaendelea vema.

Selemani atafanyiwa upasuaji wa pili mwezi Mei mwakani katika Hospitali hiyo ya CCBRT ambapo gharama zote hutolewa na Hospitali hiyo.

Na Mbeya yetu

Related

KESI YA KIKATIBA: PINGAMIZI LA AG DHIDI YA KUBENEA, WANASHERIA LATUPWA

DAR ES SALAAM Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana imetupilia mbali pingamizi la awali lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) dhidi ya kesi ya kikatiba inayohoji uhala...

MRADI WA TEDAP KUTATUA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA UMEME JIJINI DAR

 Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mfumo wa usambazaji umeme kwenye Moja kituo cha M...

BUNGE LAREKEBISHA KANUNI KUWARUHUSU WAJUMBE WALIOKO NJE WAPIGE KURA

BUNGE Maalum la Katiba limepitisha marekebisho ya Kanuni ili kuliwezesha kufikia hatua ya mwisho ya upigaji kura kuanzia tarehe 29 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba mwaka huu. Hatua hiyo ilileng...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904821
item