SAKATA LA MTOTO ALIYEWEKWA KWENYE BOX MIAKA 4 LAZUA SURA MPYA, NYUMBANI KWA MTUHUMIWA LAKUTWA SHIMO KUBWA LA MAJI

  Nasra akiwa na mama anayemlea kwa sasa Josephin Joel kutoka kambi ya ya wazee ya Fungafunga iliopo mjini hapa, akiwa katika chumba c...

 Nasra akiwa na mama anayemlea kwa sasa Josephin Joel kutoka kambi ya ya wazee ya Fungafunga iliopo mjini hapa, akiwa katika chumba cha ICU hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu baada ya kufichwa katika box kwa miaka 4 na mama yake mkubwa Mariam Said baada ya mama yake mzazi kufariki mwaka 2010.
 Hali ya Narsa kwa sasa imezidi kutengemaa ,kunawili na kuonekana kama mtoto mwenye nuru kama anavyoonekana tofauti na alivyookolewa kutoka katika box siku tano zilizopita hapo mama huyo mlezi akimpatia chakula iana ya wali na samaki anaopendelea Nasra.

 Peter Mwita Mtetezi wa haki za watoto mkoa wa Morogoro akiwa na Nasra katika kitanda anacholala mtoto huyo kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro. Alishukuru vyombo vya habari kwa kutoa habari zilizofanya Nasra kupatiwa misaada mbalimbali.
Hapo Nasra akiwa ameshika kikombe kwa mikono yake mwenyewe ilioonekana awali kutokuwa na nguvu baada ya kuomba maji ya kunywa.

MOROGORO
SAKATA la Mtoto aliyeishi katika box kwa miaka 4 sasa limechukua sura mpya baada ya nyumbani kwa mama mkubwa wake Mariam Said kukutwa kuna shimo kubwa lililojaa maji hali inayozidi kuwachanganya wakazi wa mjini hapa.


Wakiongea na mwandishi wa habari hizi mwenyekiti wa mtaa wa Azimio anakoishi mama huyo , Tatu Mgagala alisema Mei 22 polisi walifika mtaani hapo wakiwa na mtuhumiwa huyo na kukuta mlango umefungwa na kuamua kuvunja ili waweze kuingia ndani kuangalia mazingira ya nyumba hiyo.


Alisema baada ya kuingia ndani ya chumba cha Mariam walikuta kuna giza nene kutokana na chumba hicho kuzibwa na mabox na hivyo kutoa mabox hayo .


Alisema baada ya kutoa mabox hayo waliona shimo kubwa lenye maji karibu na eneo lilipo box alikokuwa akiishi mtoto huyo na alipoulizwa mama huyo kulikoni na kuacha maji ndani huku akijua kuna ugonjwa wa Dengue alidai maji hayo huyatumia kunawa miguu na mikono usiku kabla ya kulala.


‘’ Ndani ya nyumba hiyo sehemu zote zimesakafiwa isipokuwa eneo hilo ambalo lilichimbwa shimo hilo’’ alisema. Mwenyekiti huyo.


Hata hivyo imebainika kuwa mariamu na mumewe kwa muda mrefu walikuwa hawajaoga na hivyo kulazimishwa kuoga wakiwa mbaroni .


Kwa upande wake mtetezi wa haki za watoto Petter Mwita alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mei 26 mwaka huu ni Mariam ,mumewe Mtonga Omari na baba mzazi wa mtoto huyo Rashid Mvungi.


Alisema ndani ya nyumba ya mama huyo zikukutwa picha ambazo zinaonyesha kuwa mtoto huyo alikzaliwa akiwa hana ulemavu na kwamba inadaiwa ulemavu huo alipata kutokana na ukatili alikofanyiwa na walezi hao


‘’ Vitendo walivyofanya wote hawa watatu ni vya kikatili na vinatakiwa kupigwa kwa nguvu zote nah ii itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii.


Alisema baadhi ya mitandao ya kijamii ilivumisha kuwa mtoto huyo alinyanyasika na mama yake mkubwa huyo kwa madai kuwa mama yake mzazi alikufa na ugonjwa wa Ukimwi ambapo alisema suala hilo kwa mtoto huyo halipo kwani tayari alishafanyiwa kipimo hicho na kubaini hana ugonjwa huo.


Hata hivyo alisema kwa sasa wamemtafuta mama mlezi wa Mtoto huyo kwaajili ya kumuhudumia katika huduma zote na anlipwa kwa kazi hiyo.


Naye Josephina Joel mama ambaye kwa sasa ndiye anamlea mtoto huyo alidai yeye amechukuliwa kutoka katika kambi ya kulelea wazee Fungafunga ya mjini hapa na kwamba anajua uchungu wa watoto hivyo kwake anaona hakuna changamoto zozote anazopata kwa mtoto huyo.


‘’ Mimi niliachwa na mume wangu naishi Fungafunga nalelewa na Ustawi wa jamii kwangu kumlea mtoto huyo nachukulia kama mjukuu wangu na nafurahia na sioni shida yeyote’’ Alisema.


Aidha alisema mtoto huyo hupendela kula chipsi mayai, wali nyama au samaki pamoja na juice huku akionyesha kukataa ugali wala maziwa.


Mtoto huyo kama kitu hataki anafumba macho, kwa mfano ukimwambia nikupe ugali anakataa, au maziwa , lakini pia hapendi kuoga na ukimwambia kuoga au kula vyakula asivyotaka anakwambia badae’’ Alisema


Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kufika nyumbani kwa Mvungi Kihonda eneo la Maduka kumi anakoishi na mkewe wa ndoa kwa lengo la kutaka kujua jinsi huyo mke alivyochukulia jambo hilo na kuwafukuza waandishi wa habari kwa madai ya kuwa wakaandike wanavyojua wao.


‘’ Ehe waandishi wa habari mnataka nini tena kwangu uwiiii, mimi sijui chochote, ondokeni, huku akiondoka kueleka sebuleni alikokuwa mgeni wake aliyemtambulisha kama wifi yake huku akimwambia kwa lugha ambayo ilisikika kwa neno lililoashiria wandishi wa habari hao’’ Alisema 

Hata hivyo waandishi wa habari walifika nyumbani hapo nao wakiwa nyuma yake wakarudi naye hadi eneo alipo wifi yake na kujaribu kudadisi zaidi jambo bila mafanikio zaidi ya kutawala kimya kwa muda wa dakika kumi na ndipo alipohoji tena kuwa wanataka nini. 

Kamanda wa polisi mkoani hapa alithibitisha kukamatwa kwa baba wa Nasra Said na kwamba yuko nje kwa dhamana na aatafikishwa mahakamani pamoja na watuhumiwa wezake Mei 26 mwaka huu.

Related

OTHER NEWS 3262090986573523831

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item