TAARIFA ZA JESHI LA POLISI KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA DODOMA

Kutoka Dodoma Mei 05 majira ya saa saba mchana kulitokea vurugu zilizoanzishwa na wabeba mizigo wa Mji mdogo wa Kibaigwa ambapo taari...


Kutoka Dodoma Mei 05 majira ya saa saba mchana kulitokea vurugu zilizoanzishwa na wabeba mizigo wa Mji mdogo wa Kibaigwa ambapo taarifa inasema zilikua ni vurugu zilizosababisha magari kadhaa kuvunjwa vioo.

Miongoni mwa magari yaliovunjwa vioo ni pamoja na la Mbunge wa Tanga Omary Nundu, gari la Polisi na basi linalofanya safari zake kati ya Dar na Mwanza la Shabaha mbali na kuvunjwa kwa magari hayo pia maduka yaliporwa na hata barabara kuu ya Dodoma-Morogoro ilifungwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma David Misime amesema Mpaka sasa jeshi la polisi linawashikiliwa watu 34 ambao ni wakazi wa kibaigwa kata ya kibaigwa wilaya ya kongwa kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu mali.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo inasema vijana zaidi ya 300 wakishirikiana na wabeba mizigo wa Kibaigwa walifanya maandamano yasiyo na kibali na kung’oa bango la halmashauri ya kongwa lililokua na tangazo la kukataza wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru.
Baada ya bango hilo vijana hao waliamua kufunga barabara kuu ya Dodoma Morogoro kwa mawe na kuchoma matairi baadae walivamia maduka na kupora vinywaji na kuvunja majokofu.
Chanzo cha vurugu hizo  ni wabeba mizigo wa soko la mazao Kibaigwa  kupinga kitendo cha Halmashauri ya Kongwa kuweka tangazo la kutoza ushuru wa mazao sokoni hapo wakidai kwamba inawakosesha kufanya kazi zao kwani wateja wao wanashindwa kuingiza mazao sokoni.
 

Related

OTHER NEWS 3947401435443155855

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item