ANDREW CHENGE: SERIKALI IMEKOSA UBUNIFU VYANZO VYA MAPATO
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge amesema Serikali imekosa ubunifu na haitaki kupokea ushauri kuhusiana na vyanz...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/andrew-chenge-serikali-imekosa-ubunifu.html
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge amesema Serikali imekosa
ubunifu na haitaki kupokea ushauri kuhusiana na vyanzo vipya vya
mapato.a uchumi kwa mwaka 2013, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka
2014/15 pamoja na utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2013/14, Chenge
alisema kuongeza ushuru katika bia, soda, juisi na vinywaji vikali,
kumepitwa na wakati.
Wakati Chenge akieleza hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaja vyanzo mbadala vya mapato vinavyofikia Sh6 trilioni.
Katika
taarifa yake, Chenge alisema mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 2013/14,
Bajeti ilikuwa pungufu kwa Sh2 trilioni, huku Bajeti ya mwaka 2014/15
ikiongezeka kwa asilimia 8.8 (trilioni 1.6), huku ikiwa na deni la Sh1.3
trilioni ambalo halikuingizwa katika Bajeti ya mwaka 2014/15.
“Hali hii
inaweza kutafsiriwa kuwa Bajeti ya mwaka 2014/15 tayari ina pengo la
Sh4.9 trilioni. Yaani Sh2 trilioni ambazo hazikupatikana mwaka wa fedha
2013/14 na Sh1.6 trilioni ambayo imeongezeka ikilinganishwa na bajeti ya
mwaka jana na deni la Sh1.3 trilioni.
“Kuna
umuhimu wa kuharakishwa kuletwa bungeni sheria ya bajeti itakayofanya
kazi sambamba na sheria mpya ya ununuzi ili kudhibiti matumizi mabaya
kwa nia ya kuweka nidhamu katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali,”
alisema Chenge.
Alisema
wakati Serikali ikiwa haina vyanzo vya uhakika vya mapato, Deni la Taifa
lililofika Sh30 trilioni sawa na asilimia 57 ya pato la taifa ni mzigo
wa taifa na tishio kwa utengamavu wa uchumi jumla.
“Uwiano
uliopo wa Deni la Taifa na Pato la Taifa kiuchumi siyo wa kuridhisha.
Ukubwa wa deni hili hauwiani na kiwango cha uzalishaji mali na ukuaji wa
uchumi wa sasa wa asilimia 7.0,” alisema na kuongeza:
“Yalifanyika
manunuzi ya Dola za Marekani 810,000 katika Mamlaka ya Bandari Tanzania
(TPA) ambayo hayakupata kibali cha Mlipaji Mkuu wa Serikali.”
Alisema
tatizo la kutokusimamia kwa umakini matumizi ya Serikali lilisababisha
Bajeti ya mwaka 2013/14 kuanza na deni Sh611.4 bilioni, ambazo ni
matumizi ya mwaka wa fedha 2012/13 na kwamba deni hilo halikuingizwa
kwenye bajeti ya 2013/14... “Hali hii inatarajiwa pia kujitokeza tena
kwa kiwango kikubwa zaidi kwenye bajeti ya mwaka 2014/15. Malimbikizo ya
madai hayo hadi Desemba 2013, yalifikia Sh2 trilioni sawa na asilimia
nne ya pato la taifa. Tatizo hili ni lazima litafutiwe dawa haraka,”
alisema Chenge.
Alisema
ongezeko la Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15 kwa Sh1.605 trilioni,
ikilinganishwa na Bajeti ya Serikali inayomalizika ya mwaka 2013/14
linatia shaka iwapo malengo ya ukusanyaji na matumizi yatafanikiwa.
Alisema
katika mwaka wa fedha 2013/14 utekelezaji wa bajeti katika baadhi ya
mafungu ulifanyika kinyume na matarajio ya Serikali, kwa maelezo kuwa
yapo baadhi ya mafungu ambayo hayakutengewa fedha lakini walipewa fedha
nje ya bajeti za fungu husika.