MNUNUZI WA NYUMBA/KIWANJA JIHADHARI SERIKALI ZA MITAA HAWARUHUSIWI KUSIMAMIA MIKATABA KISHERIA.
Na Bashir Yakub Wiki iliyopita niliandika kuhusu Asilimia kumi ambayo serikali za mitaa huwa wanaidai hasa maeneo ya ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2015/01/mnunuzi-wa-nyumbakiwanja-jihadhari.html
Na
Bashir Yakub
Wiki
iliyopita niliandika kuhusu
Asilimia kumi ambayo serikali za mitaa huwa
wanaidai hasa maeneo ya mijini baada
ya wahusika kuwa wameuziana nyumba au kiwanja. Nikasema wazi
kabisa bila kungata
meno kuwa hiyo
pesa iitwayo asilimia kumi au pesa nyingine yoyote mtu
atakayolipa serikali za
mitaa eti kwakuwa amenunua au ameuza
eneo lake
ni rushwa. Na leo nakumbusha na kusisitiza
tena kuwa Watanzana
wajue ukitoa pesa
ile umetoa rushwa
na huyo kiongozi wa
serikali za mitaa uliyempa amepokea rushwa kwakuwa
malipo hayo hayatambuliwi
na hayaainishwi na sheria yoyote. Lazima ifike hatua
haya mambo yaeleweke. Pia
nimetahadharisha mara nyingi kuhusu
umakini unaponunua kiwanja/nyumba
na kueleza baadhi ya mambo ambayo
ukiyafanya utakuwa umefanya manunuzi salama na utakuwa umeepuka migogoro
na hata mgogoro ukitokea wewe hautapoteza. Anayetaka kusoma haya
yaliyopita aandike neno MAKALA
SHERIA kwenye google ataona makala hizo. Leo tena naeleza uhalali kisheria wa serikali za mitaa
kusimamia mikataba.
(
a ) KISHERIA HAIRUHUSIWI SERIKALI
ZA MITAA KUSIMAMIA
MAUZO YA NYUMBA/KIWANJA.
Kwanza
nataka
nieleweke wazi kuwa nazungumzia sana
ununuzi wa nyumba /viwanja kwa kuona
huruma jinsi watu wanavyopoteza umiliki
wa maeneo yao waliyonunua kwa
kuamini wameyanunua kihalali kumbe kuna nukta
walizokosea katika taratibu za
kimanunuzi na sasa zinawagharimu. Ninayosema hapo yanatokea karibia
kila siku mahakamani. Watu wanalia
lakini mda huo huna wa
kumlilia.Nianze hivi kisheria
Wakili ndio mtu ambaye anaruhusiwa kusimamia mkataba . Wakili ana
vyeo vitatu, kwanza ni wakili, pili mthibitishaji wa umma (
notary public) tatu
ni afisa wa viapo. Uwakili nao ni
cheo katika vyeo alivyonavyo wakili.
Vyeo viwili yaani uwakili na
uthibitishaji wa umma ndivyo humpa mamlaka
ya kusimamia mikataba. Hapa naongelea nyumba/viwanja lakini kimsingi
vyeo hivi si tu humpa mamlaka ya kusimamia
mikataba ya viwanja/nyumba lakini
pia mikataba yote. Hakuna katka nchi hii sheria yoyote
ambayo imemruhusu kiongozi wa serikali za mitaa kusimamia
mkataba, uwe wa nyumba, mkopo au
wowote ule hata wa mauzo
ya baiskeli. Kama hakuna sheria
hiyo maana yake ni kuwa kusimamia mikataba
si kazi yao. Kwa maana hii hii narudia kusema na
kusistiza kuwa hairuhusiwi serikali za mitaa
kusimamia mauzo ya nyumba/kiwanja.
(
b ) MKATABA
WANGU WA MANUNUZI
YA NYUMBA/KIWANJA UMESIMAMIWA
NA SERIKALI ZA MITAA JE UNA
HADHI GANI?.
Kama ndani kwako una mkataba wa manunuzi ya nyumba/kiwanja ambao ulisimamiwa na serikali za mitaa basi ujue
kuwa
mkataba huo hadhi yake ni sawa
na umesimamiwa na jirani yako ,
ndugu yako au mtu mwingine yeyote unayemuamini
ambaye amekusaidia kukamilisha
mkataba. Tuache kuishi kwa
mazoea hii ndiyo
hali halisi kisheria.
Mkataba wa mauzo ya nyumba/viwanja au mkataba
mwingine wowote uliofanyika serikali za mitaa
ni sawa na
mkataba uliofanyika nyumbani
kwako. Hiyo ndio hadhi au nafasi
ya mkataba wa aina hiyo kisheria.
Kiongozi yeyote wa serikali za mitaa anaweza kuwa shahidi yako ukiamua kumuita lakini lazima ujue kuwa ushahidi wake
katika mkataba wako kisheria
ni sawa na ushahidi wa mtu
mwingine yeyote. Hakuna eti kwakuwa
huyu au hawa ni
serikali za mitaa
kwahiyo wakionekana katika mkataba
wangu ndio utakuwa na uzito na
wenye kuaminika zaidi,
hapana. Hawa kama utaamua kuwashirikisha maana hata
kuwashirikisha nayo ni hiari
yako wanaweza kuwa
mashahidi sawa na shahidi ndugu yako au jamaa yako
mwingine yeyote . Anayeufanya
mkataba kuwa na
uzito mbele ya macho ya sheria
ni wakili na huyu ndiye aliyepewa kazi hii. Kwa hiyo wanunuzi wa viwanja/nyumba
jihadharini kwakuwa serikali za mitaa kisheria hilo si
jukumu lao. Wanayo majukumu
yao lakini hili si miongoni mwa hayo. Watu
wasifanyiwe utapeli serikali
haisimamii mikataba ya watu binafsi. Kama
serikali kuu haiwezi kusimamia mkataba
kati Bakhresa na Mohammed enterprise hata
serikali za mitaa
hawezi kusimamia mkataba kati
yangu na wewe. Nawatahadharisha zaidi wanunuzi kwakuwa
upande wa ununuzi ndio upande wa kupoteza linapotokea tatizo.
(
c ) USHAURI
KWA WANUNUZI WA
NYUMBA/VIWANJA.
Kama
unataka kununua nyumba/kiwanja na unataka mkataba
wako wa manunuzi uwe na
nguvu na hadhi ya usimamizi wa kisheria basi
epuka kuwatumia serikali za mitaa
kufanya jambo hili. Serikali za
mitaa wanajua vyema kuwa
kusimamia mikataba ya kuuza na kunuua si
katika majukumu yao isipokuwa
kwakuwa hapa ndipo penye hela kuliko hata hizo posho
zao wanazopewa na serikali kuu basi hawako
tayari kulisema hili
kwa mtu yeyote.
Hili utakuja kulijua vyema ukishapata mgogoro wakati wao hawapo
tena
wameshaondoka na chao. Mikataba
ya
serikali za mitaa
haina hadhi na
wanasheria wanaichallenge sana mahakamani wakati wa
migogoro
kiasi cha kuonekana kama vile pengine hukufanya mkataba kabisa.
Migogoro ya nyumba
na viwanja ni mingi mno lakini wewe unaweza kuiepuka migogoro hiyo
ikiwa utazingatia ushauri wa kitaalam na utaepuka
kukurupuka unapotaka kununua kiwanja/nyumba. Leo nilitaka
nikuhadharishe na hilo ndugu mpendwa.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA
NA MSHAURI WA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA
HABARI LEO KILA
JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
Source: Michuzi