BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' APATA LESENI YA BOXING
Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi leseni ya ngumi bondia...
akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa bondia huyo Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yassini Abdalla 'Ostadhi' amesema leseni ni jambo la muhimu sana kuwa nayo bondia kitu ambacho kila bondia anatakiwa kuwa nayo ambapo ndio hinaweka kumbukumbu yako ya mapambano yako yote uliocheza ndani na nje ya nchi kitaifa na kimataifa
hivyo ni kitu muhimu sana leo hii natoa leseni kwa bondia Class kwa kuwa natambua kazi yake na uwezo wake akiwa katika uringo ambapo itamsaidia kwa ajili ya kazi yake kumbuka hii ni ajira hapa kajiajiri mwenyewe' mtaji wa masikini nui nguvu zake mwenyewe'
nae bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' alishukulu kwa kusema leseni itamuongezea chachu ya kupigana vizuri zaidi awapo uringoni kwani ngumi ndio mchezo anao upenda na ndio anaucheza hivyo atafanya jitiada ili aweze kufika mbali kupitia mchezo wa ngumi
bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha kutoka kambi ya Ilala likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Kondo Nassoro, Sako Mtulya na Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye ana msimamia katika mapambano yake mbalimbali na kumpatia ushauri wa jinsi gani ya kupigana na watu anaokabiliana nao awapo uringon