Profesa Lipumba , Maalim Seif wachaguliwa tena Mwenyekiti na Katibu Mkuu CUF, Juma Duni Makamo mwenyekiti
Aliyekuwa katibu mkuu wa CUF SEIF SHARIF HAMAD akiomba kura kupata nafasi hiyo kwa mara nyingine tena katika uchaguzi mkuu wa cham...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/profesa-lipumba-maalim-seif-wachaguliwa.html
Aliyekuwa
katibu mkuu wa CUF SEIF SHARIF HAMAD akiomba kura kupata nafasi hiyo
kwa mara nyingine tena katika uchaguzi mkuu wa chama hicho
uliofanyika jana ndani ya ukumbi wa ubungo plaza jijini Dar Es Salaam.
Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho
Profesa Ibrahim Lipumba akiwa anajadili jambo na mgombea mwezake kabla
ya wajumbe kuamua nani wampe tena uenyekiti wa chama hicho cha CUFuliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Uchaguzi wa kuwapata wawakilishi katika
mkutano mkuu wa chama hicho tayari umemalizika na tayari wajume hawa
ndio wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha wananchi CUF waliochaguliwa
Viongozi
wakuu wa CUF wakionyesha mshikamano baada ya kuchaguliwa kukiongoza
chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Wa pili kulia ni
msimamizi wa uchaguzi huo Awadh Ali Said.
Na: Hassan Hamad (OMKR)
Mkutano
Mkuu wa CUF Taifa umemchagua tena Katibu Mkuu wa Chama hicho kuendelea
na wadhifa huo kwa kupata kura 675, sawa na asilimia 99.5 ya kura
zilizopigwa.
Mkutano
huo pia umemchagua Prof. Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa
kwa kupata kura 659 sawa na asilimia 95.5 na kumshinda mpinzani wake Chifu Lutalosa Yemba aliyepata kura 30 sawa na asilimia 4 nukta 3.
Aidha
mkutano huo umemchagua Mhe. Juma Duni Haji kuwa Makamu Mwenyekiti wa
Chama hicho kwa kupata kura 662 sawa na asilimia 99.25.
Akizungumza
baada ya kutangazwa mshindi Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif
Sharif Hamad, amewapongeza wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumpa tena ridhaa
ya kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Wakati wa Kampeni.
Mapema
akizungumza katika kampeni za kuomba kuchaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu
wa Chama hicho, Maalim Seif amesema siri ya mafanikio yake kisiasa ni
kutokana na kujiamini kwake kuwa kiongozi, kuwa mkweli na kuwa na
dhamira njema kwa wananchi.
Akijibu
hoja za wajumbe wa mkutano huo Maalim Seif amewataka viongozi wa chama
hicho kutotangaza kuhudhuria kwa viongozi wa kitaifa kwenye mikutano ya
hadhara hadi pale wenyewe watakapothibitisha kuhudhuria, ili kuepusha
wananchi kutoamini utendaji wa viongozi hao.
Mgombea
wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Juma Duni Haji
amesema iwapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo atashirikiana na viongozi
wengine wa kitaifa pamoja na wananchi kuhakikisha kuwa chama kinapata
maendeleo zaidi.
Chifu Yemba amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kutetea demokrasia ya kweli ndani ya chama na taifa kwa ujumla.
Chifu Yemba ambaye ni mwanasayansi kitaaluma, pia ni Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Prof. Lipumba amesema akichaguliwa atahakikisha anatembelea nchi nzima kuimarisha chama kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Aidha
amesema atafanya juhudi za ziada kuona kuwa Tanzania inakuwa na
Muungano wa kuheshimiana baina ya pande mbili za Muungano (Tanzania Bara
na Zanzibar).
Amesema wanawake watapewa nafasi ndani ya kamati tendaji ya chama kuondosha dhana ya mfumo dume unaodaiwa kuwepo katika ngazi za juu za uongozi.
Mgombea
mwengine wa nasafi ya Mwenyekiti wa CUF Taifa M’bezi Adam Bakar,
amejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na kubakia wagombea wawili wa
nafasi ya Mwenyekiti.
Mwakilishi
wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliteuliwa kuwa
mwenyekiti wa muda wa kuongoza uchaguzi huo uliosimamiwa na mwanasheria
Awadh Ali Said.