WATOTO WAWILI WALIPULIWA KWA PETROLI
Mtoto Dora Kaitaba (2) wakati wa uhai wake. Mtoto Nuru Kaitaba (3) enzi za uhai wake. Mama mzazi wa wa watoto hao (a...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/watoto-wawili-walipuliwa-kwa-petroli.html
Mtoto Dora Kaitaba (2) wakati wa uhai wake.
Mtoto Nuru Kaitaba (3) enzi za uhai wake.
Mama mzazi wa wa watoto hao (aliyenyosha mikono) akiwa na simanzi kwa kuwapoteza wanaye.
...Ndugu na jamaa wa karibu wakiwaaga watoto hao.
WATOTO wawili wa familia moja, Nuru (3) na Dora Kaitaba (2), wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kubaki majivu baada ya moto mkubwa uliotokana na petroli kulipuka nyumbani kwao, Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.Tukio hilo lililowaliza wengi, lilijiri saa tatu usiku, Jumapili iliyopita watoto hao wakiwa ndani na baba yao.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, baba mzazi wa watoto hao, Kaitaba ambaye ni mpiga
picha wa kujitegemea, alikuwa amerejea kutoka Bunju B alikofuata petroli
ambayo huiuza katika vipimo vidogo vya kwenye makopo ya maji nyumbani
hapo.
Ilizidi kudaiwa kuwa alipofika kwake
alishusha mzigo wa mafuta, watoto wake hao walikuwa wamelala katika
kibanda chake cha biashara.
Ghafla, mashuhuda wanasema, umeme
ulikatika hali iliyomfanya Kaitaba kuchukua mshumaa na kuuwasha ili
andelee na shughuli zake za kuhudumia wateja.
“Baada ya kuwasha mshumaa, moto huo ulidakwa na petroli hiyo iliyokuwa kwenye dumu na kusababisha mlipuko mkubwa.
Mashuhuda
walisema Kaitaba alikimbia kutoka bandani, lakini alipopata akili ya
kuwaokoa watoto wake tayari moto ulishakuwa mkubwa na hivyo kumfanya
apige kelele za kuomba msaada.
Hata hivyo, majirani walishindwa kuingia ndani kutokana na ukubwa wa moto huo na uduni wa vifaa vya kuzimia.
Watu wakiwa wanaangalia tukio hilo kwa
masikitiko makubwa, Kikosi cha Zimamoto Bagamoyo kiliwasili kikiwa
kimechelewa hivyo kuambulia kuchukua majivu ya watoto hao wawili
waliaochana mwaka mmoja kuzaliwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP
Onesphory Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema tofauti
na madai ya baadhi ya watu kuwa baba mzazi wa watoto hao anashikiliwa na
polisi, alichukuliwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kutibiwa
majeraha na hatachukuliwa hatua yoyote kwa vile kilichotokea ni ajali.
Aidha Kamanda Matei alitumia fursa hiyo
kupiga marufuku biashara hiyo ya mafuta ya petroli na dizeli ambayo ni
maarufu wilayani humo.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.