KOMBORA LALIPUA MATENKI YA MAFUTA
Vikosi vya zima moto vya Libya vinapambana kujaribu kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua tanki la kuhifadhia mafuta wakati ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/kombora-lalipua-matenki-ya-mafuta.html
Vikosi vya zima moto vya Libya vinapambana kujaribu
kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua tanki la kuhifadhia
mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika
mji mkuu Tripoli. Tanki hilo ni miongoni mwa matanki yanayomilikiwa na
Kampuni ya mafuta ya serikali ya Libya yenye lita milioni sita za
mafuta.
Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.
Serikali ya muda ya Libya imetaka ustishaji wa
mapigano katika eneo hilo la maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto
kufanya kazi yao bila kuingiliwa.