MKASA WA MOTO GEREZANI RWANDA: WATU 3 WAUAWA

Watu watatu wamefariki na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa wakati gereza moja liliteketea moto magharibi mwa Rwanda, karibu na mpaka w...



Watu watatu wamefariki na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa wakati gereza moja liliteketea moto magharibi mwa Rwanda, karibu na mpaka wa DRC.
Tukio hili linatokea mwezi mmoja baada ya gereza jengine, Muhanga, kuteketea moto katika jimbo lililopo kusini mwa Rwanda.

Ajali hiyo ya moto imeripotiwa kutokea majira ya jioni (Jumatatu) katika gereza la Nyakiriba, katika wilaya ya Rubavu mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 Akiongea na BBC kwa njia ya simu mkuu wa wilaya hiyo, Sheikh Hassan Bahame, amesema kuwa juhudi za uokozi zimefanyika haraka ila mahabusu 3 walifariki na wengine 44 kupatwa na majeraha ya moto.
Majeruhi walifikishwa mara moja katika hospitali kuu ya wilaya.
Amesema kuwa kutokana mazingira ya milima ambapo gereza hilo limejengwa, imekuwa vigumu kwa wazima moto kufanya kazi yao kwa wepesi na haraka.

Shekh Bhame ameelezea hasara iliyojitokeza.'' Hasara kubwa abayo imetokea ni kifo cha hawa wafungwa. Na majeraha waliyopata wafungwa wengine. Kuna vitu vingi vimeharibika na hatujajua idadi yake bado.''
Sheikh Bahame ametahadharisha kuelekeza lawama la shambulio la kigaidi akisema kuwa japo inatia shaka, ni muhimu uchunguzi zaidi kufanywa.

''Hata sisi tunajiuliza, mbona mambo haya yametokea, na juzi tu yametokea Muhanga?Inatakiwa uchunguzi wa ndani zaidi ufanywe. Lakini uhakika bado hatujapata.'' Amesema Sheikh Bahame.
Uchunguzi umeanzisha kujua chanzo cha moto, pamoja na ule moto katika gereza la Muhanga mwezi mmoja uliopita.

Related

TUJUZANE 4383335242327396797

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item