MWILI WA MWANAFUNZI WA CHUO CHA RUCO ALIYECHOMWA AKIDHANIWA MWIZI WAAGWA, POLISI WAELEZEA TUKIO KAMILI
LEMA enzi za uhai wake Baadhi ya raia walijitokeza kumuaga Lema katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/mwili-wa-mwanafunzi-wa-chuo-cha-ruco.html
LEMA enzi za uhai wake
Baadhi ya raia walijitokeza kumuaga Lema katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa.
Mwili wa Daniel Lema ukiagwa na baadhi ya wanachuo pamoja na raia waliojitokeza kuhudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu
Mwili
wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada
ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa
(Ruaha University College - RUCO) umeagwa na kusafirishwa kuelekea
mkoani kwao kilimanjaro kwa mazishi.
Wanafunzi
kadhaa wa chuo hicho na baadhi ya wananchi wa manispaa ya Iringa
waliogusa na tukio hilo walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa Iringa
ambako shughuli ya kuuga mwili huo ilifanyika.
Jeshi
la Polisi mkoani iringa linawashikilia watu wanne ambao ni walinzi
wa Juka usalama waliokuwa wakilinda nyumba moja ya kulala wageni iliyopo
kihesa katika manispaa ya iringa kwa madai ya kumchoma moto mwanafunzi
huyo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi
alisema tukio hilo lilitokea Juni 24 majira ya saa tisa usiku baada ya
wasamaria wema kutoa taarifa polisi kuwa kuna mtu anatembea akiwa
anawaka moto.
Mungi
alisema mara baada ya kupata taarifa hiyo Jeshi la Polisi lilifika
katika eneo hilo na kumkuta Daniel Lema (25) akiwa ameanguka chini
huku akiwa amefungwa mikono nyuma.
Kamanda
huyo aliwataja watuhumiwa hao waliomchoma moto kuwa ni Mussa Nganga
(28), Costa Mgayuka (38), Steven Kalole (24) na Samson Peter (24) wote
wakazi wa Kihesa waliokamatwa kabla ya kutoweka mjini iringa .
“Tulipopata taarifa tulifika eneo hilo kwa haraka na tukamkuta
ameanguka chini tulimfungua ile mikono na kumchukuza vizuri tulimkuta
akipumua kwa shida ndipo tukamkimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Iringa kwa ajili ya kupata matibabu.”alisema Kamanda Mungi
Alisema
kuwa mwanafunzi huyo alikuwa baa moja inayoitwa In box bar
inayomilikiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela
akipata kinywaji huku angiangalia michuano ya mpira wa miguu (kombe la
dunia) ambayo inaendelea nchini brazili.
“Mwanafunzi
alikuwa anaangalia michuano hiyo ya mpira wa miguu kwenye baa hiyo na
baada ya mpira huo kuisha aliondoka na kuelekea nyumbani kwake Kihesa
kabla ya kufika nyumbani eneo hilo kuna nyumba ya kulala wageni iitwayo
Glory lodge ambapo pembeni yake kuna grocery moja iitwayo Glory grocery akaingia hapo akifikiri ipo wazi ili aendeleze kinywaji,” alisema.
Alisema
wakati akigonga mlinzi wa nyumba ya kulala wageni Glory lodge ambae ni
mmasai aitwaye Mussa Nganga alimuona na kumuita ndipo kijana akakimbia
na baada ya kukimbia alimfukuza na kuwaita wenzake watatu na kumfanyia
kitendo kama hicho.”alisema Mungi .
Baada
ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Lema aliendelea na matibabu
yake mpaka alipokutwa na mauti.