SERIKALI YAPOKEA MABEHEWA 25 YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 4.3 KUTOKA INDIA
Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (katikati), akifurahia jambo wakati wa kupokea mabehewa hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/serikali-yapokea-mabehewa-25-yenye.html
Waziri
wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (katikati), akifurahia jambo wakati wa
kupokea mabehewa hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi
Kipalo Kisamfu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk.Shaaban Mwinjaka.
Waziri
wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (kulia), akiangalia moja ya mabehewa
kati ya mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto yenye thamani ya sh.bilioni
4.3 aliyoyapokea kutoka Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and
Industriles Limited ya India Dar es Salaam Leo, kwa ajili ya Kampuni ya
Reli Tanzania (TRL). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi
Kipalo Kisamfu.
Waziri Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari wakati akipokea mabehewa hayo.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na wa TRL wakishusha toka katika meli moja ya mabehewa hayo.
Fundi wa Shirika la Reli Tanzania , Ephrahim Joel akikaza nati ya moja ya mabehewa hayo.
Waziri Mwakyembe akiangalia moja ya mabehewa hayo.
Fundi
wa Shirika la Reli Tanzania , Francis Mpangala naye akikaza nati katika
moja ya mabehewa hayo. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)
Baadhi ya mabehewa hayo yakiwa yamepangwa katika njia yake bandarini baada ya kushushwa kutoka katika meli.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imepokea mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto yenye thamani ya sh.bilioni
4.316 kwa ajili ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka Kampuni ya M/S
Hindusthan Engineering and Industriles Limited ya India.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabehewa hayo Dar es
Salaam leo, Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe alisema mabehewa
hayo ni sehemu ya mpango kabambe wa Serikali wa kufufua Kampuni ya Reli
Tanzania chini ya mapngo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa (BRN).
Alisema
mpango wa BRN kwa Kampuni ya Reli Tanzania umelenga kuiwezesha kampuni
hiyo kiutendaji ili iweze kusafirisha tani milioni 3.0 ifikapo mwaka
2016 kutoka tani 200,000 zilizosafirishwa mwaka 2012 kupitia Reli ya
kati.
"Katika
harakati za kufikia malengo haya makubwa, Serikali kupitia bajeti zake
za mwaka 2012/2013 na 2014, ilitenga fedha kwa ajili ya kugharamia
miradi mbalimbali iliyolenga kuboresha vitendea kazi vya Kampuni ya Reli
Tanzania" alisema Mwakyembe.
Alitaja
miradi iliyopangwa ni pamoja na kujenga upya vichwa vya Treni 8,
kununua vinchwa vya treni vipya 13, mabehewa mapya 274 ya kubebea mizigo
na mabehewa ya breki.
Mwakyembe
alitaja mradi mwingine ni kununua mashine ya kushindilia kokoto,
kununua mabehewa 22 mapya ya abiria na kununua mabehewa 25 mapya ya
kubebea kokoto ambayo yamepokelewa jana.
Katika
hatua hiyo Mwakyembe ametumia fursa ?hiyo kuipongeza TRL kwa kupokea
mabehewa hayo kwa wakati na kuishukuru Kampuni ya Hindusthan Engineering
and Industries Limited ya India kwa utengenezaji wa mabehewa hayo kwa
muda uliopangwa.
Alisema
lengo ni kuiwezesha TRL kufikia malengo ya kusafirisha mizigo tani 3.0
na kutembeza treni za abiria tano kwa wiki ifikapo mwaka 2016.