SUMATRA YATOA UFAFANUZI KUHUSU MALALAMIKO YA CHAKUA
Rose masaka - MAELEZO DAR ES SALAAM Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imetoa ufafanuzi kuwa ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/sumatra-yatoa-ufafanuzi-kuhusu.html
Rose masaka - MAELEZO DAR ES SALAAM
Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imetoa
ufafanuzi kuwa hajafikia muafaka wa kuwalazimisha abiria wa mikoani
kutumia mchakato wa mbinu mpya ya ukatishaji wa tiketi za mabasi ya
kwenda mikoani kwa njia ya mtandao ikiwemo wa simu za mkononi kwa kuwa
baadhi ya wamiliki wa mabasi wamegawanyika, na bado haukidhi mahitaji ya
sasa.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Meneja wa Mawasiliano wa SUMATRA, David Mziray
wakati akizungumza na mwandishi wa habari wa Idara ya Habari(MAELEZO)
baada ya Chama Cha Kutetea Abiria Tanzania(CHAKUA) kuilalamikia,
SUMATRA ndio inayochelewesha mchakato huo na wameairisha kufanyika
kikao cha wadau kilichotakiwa kufanyika Mei30,mwaka huu.
Malalamiko
hayo yalitolewa na Mwenyekiti wa CHAKUA, Hassan Mchanjama, alipokuwa
akiongea na katika mkutano na waandishi wa habari,uliofanyika leo kwenye
ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).
Aidha
kutokana na malalamiko hayo, Mziray alisema ni kweli kikao hicho,
kiliairishwa kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika huku akisisitiza
kikao hicho kilikuwa cha mashauriano na si cha kutoa uamuzi.
Mziray
aliongeza kwamba , hata hivyo baadhi ya wamiliki wa mabasi hayo,
wamegawanyika kwani wapo wanaouunga mkono utaratibu huo na wengine
wanaupinga kutokana kwamba watakosa abiria , upatikanaji wa fedha
unachukua muda mrefu na mapato yao yatajulikana.
“Hatuwezi
kuulazimisha utaratibu huo utumike kwa sasa kwa sababu nilizotaja na
pia kuna baadhi ya wananchi hawatumii simu za mkononi,” alisema
Mziray.
Mziray
alisema waliishauri CHAKUA watoe elimu kwa wamiliki hao ili kuwezesha
utaraibu huo utumike kwa wale wanauunga mkono na wanaoweza kuutumia,
bali kwa abiria ambao ni vigumu kutumia utaratibu wa zamani utumike.
CHAKUA
iimetoa malalamiko hayo kwa mamlaka hiyo baada ya kuwasilisha
mchakato huo kwa kumwandikia barua , Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison
Mwakyembe , ambapo uongozi wa chama hicho ulidai kuwa aliiagiza
SUMATRA kuitisha kikao na wadau .
Kikao
hicho kiliitishwa Desemba 17,mwaka huu ,ambapo wadau hao ambao ni
Wamiliki wa Mabasi(TABOA), CHAKUA na Jeshi la Polisi la Usalama
Barabarani walikubaliana kuanzishwa kwa mchakato huo kwa kukiitisha
kikao na wadau baada ya miezi mitatu.
Aidha
Mchanjama amesema kuwa utaratibu waliougundua ni mzuri na wenye manufaa
kwa wamiliki , abiria na Serikali kwani itarahisisha muda wa kukata
tiketi bila kwenda kituo cha mabasi.
Ameongeza
kwa kusema kuwa nauli zitakuwa ni halali na zilizoainishwa na SUMATRA
ili kuondoa kero kwa abiria ya kuongezewa nauli hususani siku za sikukuu
au shule zikifunguliwa au kufungwa.
“Utaratibu
huu unarisisha abiria kudai fidia pindi anapopata madhara katika mabasi
kama ajali ,kupotelewa na mzigo na magari kugoma” alisema Mchanjama.
Aliongeza
kuwa kila kitu kitakuwa wazi katika mtandao, hivyo ni rahisi kwa abiria
kupata nyaraka za basi husika pindi anapopata tatizo,pia mmiliki
atafaidika kwa kupata mapato moja kwa moja tofauti na sasa pesa zinapita
mikononi mwa watu wengi.
Kuna
taasisi nyingi za serikali na watu binafsi ambazo zimekuwa mfano mzuri
katika utumiaji wa mtandao ambazo ni TRA,TANESCO,DAWASCO na Benki
mbalimbali.