TAARIFA YA MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI KUHUSU BOMU LILILOLIPUKA ARUSHA
Jumatatu July 07 kwenye moja ya migahawa iliyopo eneo la Uzunguni Jijini Arusha,Watu wanane waliripotiwa kujeruhiwa katika mlipuko...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/taarifa-ya-mkurugenzi-wa-makosa-ya.html
Jumatatu
July 07 kwenye moja ya migahawa iliyopo eneo la Uzunguni Jijini
Arusha,Watu wanane waliripotiwa kujeruhiwa katika mlipuko wa
bomu.Mkurugenzi wa makosa ya jinai wa Jeshi la Polisi Kamishina Issaya
Mngulu amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa nane usiku ambapo
watu wasiojulikana walirusha bomu hilo ndani ya mgahawa ujulikanao
kamaVama Traditional Indian Cusino uliopo jirani na viwanja vya Gymkhana
jijini Arusha.Pamoja na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Jeshi la
Polisi za kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na usalama na yenye
tulivu,bado kumeendelea kuwa na matukio ya kiuhalifu yakiwemo ya
milipuko katika maeneo mbalimbali.
Mkurugenzi
wa makosa ya jinai anasema “Kufuatia kutokea kwa matukio haya
bado tunaendelea na upelelezi wa kina ili kuhakikisha kwamba wale wote
walioko kwenye mtandao huo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya
sheria’
‘katika
tukio hilo la jana tayari watu wawili wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi
lakini pia kati ya wale wanane mmoja wao hali yake siyo nzuri hivyo
amepelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi’.
Pia
ameongeza kwa kusema katika matukio mengine ya nyuma yaliyowahi kutokea
mpaka sasa jumla ya watu 20 wamekamatwa wakiwemo sita wanaosadikiwa
kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea Julai 3 mwaka huu nyumbani kwa
Shekhe Ally Sudi mkoani Arusha na wengine 12 katika tukio lililotokea
Zanzibar.
Hata
hivyo Kamishina Mngulu ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa
kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, vilevile wawe makini na mtu ama
kitu watakachokitilia shaka.