MAMA TUNU PINDA AULA KUWA BALOZI WA AMANI DUNIANI JIJINI SEOUL, KOREA KUSINI
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na Mwenyekiti wa U...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/08/mama-tunu-pinda-aula-kuwa-balozi-wa.html
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu
Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas
Walsh (kushoto) na Mwenyekiti wa UPF, Dk. Charles Yang mara baada ya
kutunukiwa cheti cha kumtambua kama Balozi wa Amani Duniani katika hafla
ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana
usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA IRENE
BWIRE WA OWM).
Mke
wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia mstari wa mbele) katika
picha ya pamoja viongozi wengine waliotunukiwa vyeti vya kuwatambua kama
Mabalozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia
kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini
Seoul, Korea Kusini. Walioshika vyeti kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa
visiwa vya Samoa, Bibi Filifilia Tamasese , Mke wa Rais wa visiwa vya
Marshall, Bibi Lieom Anono Loeak na Mke wa Rais wa Fiji, Bibi Koila
Nailatikau.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu
Pinda (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja viongozi
wenzake 10 waliotunukiwa vyeti vya kuwatambua kama Mabalozi wa Amani
Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama
uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea
Kusini.(PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).