PICHA: UZINDUZI WA ALBUM YA SHIKILIA PINDO LA YESU YA ROSE MUHANDO ULIOFANYIKA JIJINI MWANZA

Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama kulia na mwimb...


Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama kulia na mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje katikati na Mwimbaji Chengula kushoto wakati wa tamasha la uzinduzi wa Albam ya Shikilia Pindo la Yesu uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza akisindikizwa na waimbaji malimbali wa muziki huo akiwemo Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia, Albam hiyo imezinduliwa na Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula ambaye alimwwakilisha Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba, Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa ujumbe aliouwakilsha katika uzinduzi huo kutoka kwa Mh. Januari Makamba Mabula ameuelezea ujumbe huo kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kushawishi makampuni ili yadhamini pia matamasha ya muziki wa injili ka ambavyo yamekuwa yakiafuturisha vikundi na waumini mbalimbali wakati wa mfungo wa ramadhan, kwakuwa muziki wa injili pia unaeneza amani na upendo kwa jamii ya watanzania, Hii itasaidia kupunguza ghara za uandaaji jambo ambalo kwa namna moja au nyingine litakuwa linarahisisha uandaaji wa matamasha hayo ambayo yamekuwa ni chachu ya watu kuachana na maovu na kuwa watu wema katika jamii.


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akigawa albam ya Rose Muhando kwa Mh. Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Maaskofu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.


 Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 Meya wa jiji la Mwanza ya Mhe.Stanslaus Mabula akinyanyua juu albam za mwimbaji Rose Muhando wakati alipozindua albam hiyo mkoani Mwanza  kwenye uwanja wa CCM Kirumba.


 Mwimbaji Bony Mwaiteje akifanya vitu vya sarakasi jukwaani.
 Miwmbaji wa kimataifa kutoka zambia Ephraim Sekereti ni mmoja wa waimbaji waliokonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa injili.
 Noa Victoria Singers wakifanya vitu vyao.




 Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kulia akiwa amesimama na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati wa uzinduzi huo kutoa kulia ni waimbaji Chengula Bony Mwaiteje , Tumaini Njole na Rose Muhando.
 Mmoja wa waratibu wa uzinduzi huo Bw. Hudson Kamoga akizunguza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Alex Msama.

Related

OTHER NEWS 184876340380920986

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item