ALEX MSAMA ATANGAZA VITA NA WEZI WA KAZI ZA WASANII, ASEMA WATASAKWA POPOTE WALIPO

M kurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam Bw. Alex Msama akimwaga furushi lililojaa CD na DVD feki za kazi mbaim...

Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam Bw. Alex Msama akimwaga furushi lililojaa CD na DVD feki za kazi mbaimbali za wasanii zinazorudufiwa kwa wizi na watu wasiokuwa waaminifu hivyo kupelekea hasara kubwa kwa wasanii, kwakuwa kazi hizo haziwaingizii kipato chochote zaidi ya kwanufaisha wezi hao, Kazi hizi zimekamatwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam ikiwa ni pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengeneza kazi hizo katika msako huo. Thamani ya CD, DVD na vifaa vilivyokamatwa ni shilingi milioni 200 katika picha anayesaidiana naye ni Afande D/SSG Daniel Gingu na wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa kituo cha polisi Urafiki ASP Egfred Kasikama kushoto na katikati ni Mkuu wa upelelezi wa kituo hicho ASP Denis Moyo.


Alex Msama amesema kazi ya kuwaska na kuwakamata wezi wa kazi za wasanii inaendelea na siyo zimamoto kama baadhi ya watu wanavyodai, ameongeza kuwa watawafuata popote walipo mpaka wahakikishe wametiwa nguvuni wahalifu hao wa kazi za wasanii,amelishukuru jeshi la polisi kwa ushirikiano linaotoa kwa kampuni yake pamoja na TRA Mamlaka ya Mapato na Wizara ya habari Vijana Utamaduni na Michezo kwa ushirikiano wanaotoa.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam Bw. Alex Msama akionyesha makasha ya picha za wasanii mbalimbali yanayowekwa kwenye CD na DVD zikiwani kazi za wizi kwa wasanii huku viongozi wa kituo cha polisi cha Urafiki wakishuhudia.

Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam Bw. Alex Msama akionyesha mashine ambayo ina uwezo wa kufyatua CD 12 kwa dakika kumi tu ambayo nayo imekamatwa katika msako huo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam Bw. Alex Msama akionyesha wino ambao hutumika kuchapisha picha mbalimbali za wasanii.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam Bw. Alex Msama akionyesha Printer inayotumika kuchapicha picha.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari na kufafanua mambo mbalimbali kuhusu msako huo unaoendelea nchini kote.

Related

TUJUZANE 6546186235184121487

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item