BUNGE LA KATIBA: KAMATI KUANZA KUWASILISHA SURA ZILIZOSALIA ZA RASIMU YA KATIBA

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma. 01/09/2014. KAMATI 12 za Bunge Maalum la Katiba kesho zitaanza kuwasilisha Sura zilizosalia...


Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
01/09/2014.
KAMATI 12 za Bunge Maalum la Katiba kesho zitaanza kuwasilisha Sura zilizosalia za Rasimu ya Katiba Mpya ambazo ni Sura ya Pili, Tatu, Nne na ya Tano kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa tangu tarehe 5 Agosti, Mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahya Khamis Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habri kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.
“Kila Kamati imeshandaa taarifa kwa ajili ya kuiwasilisha katika Bunge hapo kesho”, alisema Katibu huyo.
Aidha, Katibu huyo ameongeza kuwa baada ya sura hizo kumalizika, Sura zitakazofuata ni Sura ya Saba, Nane na 14 na nyingine ni sura mpya.

Ameongeza zaidi kuwa, utaratibu huo utaendelea mpaka sura zote zitakapomalizika siku ya tarehe 8 Septemba, 2014 saa mbili usiku.
Katibu ameongeza kuwa Bunge hilo litaanza kujadili Sura hizo za Rasimu ya Katiba Mpya kuanzia siku ya tarehe 9 Septemba, 2014.

Related

OTHER NEWS 888968637388748095

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item