TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 01/09/2014

KATIKA TUKIO LA KWANZA: MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FUNU A MAGOKO (35) MKAZI WA ITUMBI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO SEHEMU ZA KI...


KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FUNUA MAGOKO (35) MKAZI WA ITUMBI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO SEHEMU ZA KICHWANI NA WATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LUGANO GEORGE (33) NA 2. MOSSES MWACHILA (30) WOTE WAKAZI WA ITUMBI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEOMAJIRA YA SAA 00:30 HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI KULIPA KISASI KWANI INADAIWA KUWA MAREHEMU NA WENZAKE WANA TUHUMIWA KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA MAUAJI.

WATUHUMIWA WAMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 07 – 09 AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE MARA MOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.916 APD AINA YA SURF HILUX IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE KEFFA MAHENGE (29).
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.08.2014 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI HUKO MAENEO YA SOGEA – TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KATIKA TUKIO LA TATU:
DEREVA ALIYEKUWA AKIENDESHA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.495 ALM AINA YA NISSAN PICK UP ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BONIFACE MWASOBA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI HILO KUACHA NJIA NA KUPINDUKA MAENEO YA NANENANE DARAJANI JIJI NA MKOA WA MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:30 HUKO MAENEO YA NANE NANE DARAJANI, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/IRINGA. AIDHA KATIKA AJALI HILO WILLY BONIFACE MWASOBA (07) MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MKAPA ALIJERUHIWA NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. GARI LIPO ENEO LA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA DEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Related

TUJUZANE 1865310523779776695

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item