MAALIM SEIF AHUDHURIA MKUTANO WA KIMATAIFA WA UCHUMI
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif, akisalimiana na Kiongozi wa Istambuli wakati akiwasili katika ukumbi wa mkuta...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/09/maalim-seif-ahudhuria-mkutano-wa.html
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif, akisalimiana na Kiongozi wa Istambuli wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano. wa Kimataifa wa Uchumi unaofanyika nchini huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif akiwasili ukumbi wa mkutano na Ujumbe wake.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif akiwa na Mkutano na Ujumbe wake
Na Khamis Haji, Istanbul
Katika mkutano huo uliolenga kuweka mikakati ya matumizi bora ya rasilimali kwa maendeleo ya kiuchumi, zaidi ya wajumbe 500 kutoka mataifa tafauti, wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara, wataalamu wa uchumi na fedha na wawakilishi wa sekta binafsi wanahudhuria.
Amesema miongoni mwa matatizo makubwa kwa nchi nyingi ni kukosekana fursa za kiuchumi zinazoweza kuzaa ajira nyingi kwa wananchi, hali inayochangia kukosekana imani ya wananchi na baadaye kuathiri utulivu na amani ambao ni msingi wa ukuaji wa uchumi na maendeleo.
“Tukiungana mataifa ya Ulaya, Asia, America na Afrika tukiweza kuzitumia rasilimali tulizonazo katika maeneo yetu kwa kuzingatia vipaumbele vya ukuaji wa uchumi, tutaweza kuleta mabadiliko na kuunda fursa nyingi kwa wananchi katika Mabara yote”, amesema Bjorkman.
Mkurugenzi huyo amehimiza utaratibu wa mataifa kuchagua maeneo machache yenye ufanisi kushirikiana kwa mujibu wa mazingira yao, ambapo mataifa yataweza kushirikiana katika kuyaendeleza, badala ya kuweka vipaumbele vingi kwa wakati mmoja, hali ambayo haileti mafanikio makubwa katika utekelezaji wake.
Ujumbe wa Zanzibar pia unawashirikisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui, Katibu wa Tume ya Mipango, Amina Khamis Shaaban na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega uchumi (ZIPA), Salum Nassor