RAIS KIKWETE ATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI, MRADI WA NYUMBA ZA MAKAZI ZA NSSF KIJICHI
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati alipotembelea u...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/10/rais-kikwete-atembelea-daraja-la.html
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati alipotembelea ujenzi wa Daraja la Kigamboni,jijini Dar es Salaam .
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea kadi maalum ya pongezi ya siku yake ya kuzaliwa Oktoba 07,2014 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau.Rais Kikwete anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ,akiwa ametimiza miaka 64 toka kuzaliwa kwake.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangaliwa maendeleo ya ujenzi wa Daraja Kigamboni jijini Dar es Saalam,wakati alipotembelea kuona maendeleo yake.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alieambatana na Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Magufuli,Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakitembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.ujenzi huo unafanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kutembelea eneo hilo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali,Viongozi wa NSSF pamoja na wakandarasi wanaojenga daraja hilo mara baada ya kumaliza kutembelea eneo la mradi huo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa NSSF pamoja na wajenzi wa Nyumba za Makazi za shirika hilo zinazojengwa Mtoni Kijichi,jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipatiwa Maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa nyumba za Makazi zinazojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es salaam,wakati alipotembelea kujionea Maendeleo ya mradi huo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kwenye jiwe la mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Mtoni Kijichi,jijini Dar es salaam
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza kwa makini,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau alipokuwa akimfafanulia jambo kuhusu mradi huo wa Nyumba.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.
Rais Jakaya Kikwete ametembelea daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, jana, ambapo ameagiza changamoto zilizoanishwa zitatuliwe haraka kabla mradi haujamalizika.
Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya ujenzi huo, Rais Kikwete alisema utekelezaji wa mradi unapaswa kwenda sambamba na utatuzi wa changamoto hizo.
Mapema wakati akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa Mradi huo, John Msemo, alisema zipo changamoto chache ambazo zinapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano na serikali.
Alizitaja changamoto hizo kuwa pamoja na zile za wembamba wa baadhi ya barabara pamoja na msongamano wa magari.
Alitoa mfano wa barabara za Vijibweni-Mjimwema, Bendera Tatu-Kamata na Gerezani- Ohio kuwa ni nyembamba.
Pia aliutaja msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Kilwa- Mandela, Chang’ombe-Mandela na Nyerere (Tazara) kuwa unapaswa kushughulikiwa.
Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alisema tayari serikali imeanza kushughulikia changamoto hizo, ambapo imeongea na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) pamoja na kutenga fedha katika bajeti kwa ajili ya upanuzi wa barabara hizo.
Dk. Magufuli alisema katika bajeti ya mwaka huu, fedha zimetengwa kulipa fidia kwa ajili ya barabara ya Vijibweni-Mjimwema ili iongezwe upana na kwamba, ile ya Ohio-Gerezani mazungumzo yanaendelea na ADB.
Daraja la Kigamboni linalojengwa kwa ushirikiano wa serikali na wadau na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo linatarajiwa kukamilika Juni, mwakani na kuzinduliwa na Rais Kikwete.
Baada ya kutembelea mradi huo, Rais alikagua ujenzi wa nyumba 1,120 zilizojengwa na NSSF katika eneo la Mtoni Kijichi, Kigamboni, ambapo aliupongeza uongozi wa shirika hilo kwa kukamilisha mradi huo wa nyumba za watu wa kipato cha kati na chini.
Rais alizindua mradi huo na kuiagiza Manispaa ya Temeke kuangalia uwezekano wa kuijenga vizuri barabara inayokwenda mahali nyumba hizo zilipo pamoja na kutengeneza miundombinu nyingine muhimu ikiwemo maji. Mapema wakati wa ziara hiyo, Rais ambaye alisherehekea siku yake ya kualiwa jana, alikabidhiwa kadi maalumu ya kumtakia maisha marefu na Mkurugenzi Mkuu wa Nssf, Dk. Ramadhan Dau.