SULUHU KWA WAGONJWA WA FIGO NA MFUMO WA MKOJO YAPATIKANA

Watanzania  kunufaika na kile ambacho wachambuzi huona kama nafasi adimu katika sekta ya afya. Hii ni kwasababu nchi inatarajia kupokea ...

Watanzania  kunufaika na kile ambacho wachambuzi huona kama nafasi adimu katika sekta ya afya. Hii ni kwasababu nchi inatarajia kupokea wataalamu wawili kutoka taasisi mashuhuri ya matibabu duniani. Kwa kushirikiana na madaktari kutoka hosipitali ya Hindu Mandal. Madaktari kutoka hospitali ya Apollo watahudumia  na kutoa ushauri kwa wagonjwa wa figo na mfumo wa mkojo siku ya Oktoba 10 na Oktoba 11 katika Hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam.
Watanzania wengi  wenye maradhi hayo hushindwa kupata matibabu hapa nchini na  badala yake husafiri nje ya nchi kwa ushauri na matibabu. Lakini kwa sasa wanaweza kupata huduma hiyo hapa  Tanzania katika hosipital ya Hindu Mandal. Madaktari hao wawili kutoka  hosipital inayoongoza katika kutoa huduma bora duniani ya Apollo wanatarajia kutoa huduma iliyo na ubora uleule hapa nchini Tanzania. Watanzania watapata fursa ya kuonana na madaktari kati ya saa 3 kamili asubuhi  mpaka saa 8 kamili mchana siku ya Ijumaa na Jumamosi kuanzia saa 10 kamili jioni mpaka saa 1 na nusu usiku kwa gharama ya shilling 45,000 tu kwa kila mgonjwa kwa ajili ya kumuona dokta.
Ujio wa Dk. Sanjay Maitra na Dk.Rajagopal katika hosipital ya Hindu Mandal ni sehemu ya nia ya dhati ya  hospitali ya Apollo ya kutoa huduma bora za matibabu kwa wote na kujenga uhusiano mzuri na nchi ya Tanzania ambao ulianza zaidi ya miaka kumi iliyopita. Madaktari hawa wakiwa Tanzania watakuwa kuwawafuatilia  wagonjwa mbalimbali, kupitia upya kesi za magonjwa yao na kutoa ushauri juu ya matibabu kama taarifa za matibabu zinavyoeleza.
Hatua hii ni sehemu mpango mkakati  wa hospital za Apollo wa kutokomeza magonjwa kama haya nchini Tanzania. Hatua hii imechukuliwa kutokana na utafiti uliofanyika hivi karibuni. Kulingana utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO)  mwaka 2011 vifo vitokanavyo na ugonjwa wa figo nchini Tanzania vimefikia 4533 sawa na 1.03 asilimia ya vifo vyote. Takwimu hizi zimeiweka  Tanzania  katika nafasi ya 54 duniani. Ugonjwa wa figo umeripotiwa kuwa katika asilimia 14 miongoni mwa watu wazima katika hospitali kulingana ujumla idadi ya watu. Chanzo cha kifo  kwa wagonjwa hao ni  kushindwa kwa figo na mishipa ya  moyo au matatizo yanayojitokeza kutokana na ugonjwa huo. Katika utafiti mwingine uliofanyika hivi karibunina Shirika la Afya Duniani  WHO mwaka 2012 nchini  Tanzania. Wagonjwa 100 waligundulika kuwa na magonjwa sugu ya figo kutoka jumla ya wagonjwa 1,476 waliokuwa na magonjwa mbalimbali, asilimia 61 walikuwa wanaume ambapo kati yao asilimia 91 walikuwa katika ugonjwa sugu wa  figo  katika hatua ya nne na tano.
Dk. Sanjay Maitra ni mtaalamu wa magonjwa  ya figo. Anatarajia kuhudumia watanzania wenye matatizo hayo katika kuwepo kwake nchini Tanzania. Amefanikiwa katika upandikizaji wa figo kwa watu zaidi ya 500 uliofanyika chini ya usimamizi wake. Hivyo basi ana uzoefu mkubwa sana katika masuala ya figo.
Mtaalamu wa  mfumo wa mkojo  na viungo vya uzazi kwa wanaume,  Dk.Rajagopal atakuwa akihudumia  wagonjwa wenye  matatizo yanayohusiana na hayo kwa kulenga zaidi katika  upasuaji na matibabu. Wagonjwa wanaohitaji Matibabu au ushauri  juu ya jiwe katika figo, uhadubini, kufeli kwa  kibofu cha mkojo, matatizo ya mfumo wa mkojo, upandikizaji wa figo, utasa, ukosefu wa nguvu za kiume, maambukizi ya kawaida au matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa mkojo na viungo vya uzazi kwa wanaume wanashauriwa  kutokosa fursa hii iliyopo  mbele yao.
Katika kiliniki hiyo ya siku 2, wagonjwa watapimwa ili  kugundua hali yao na kushauriwa kama  wanaweza kupata dawa na tiba  ndani ya nchi ambayo itasaidia kuponya maradhi yao. Kwa upande mwingine, kulingana na ukali wa hali ya mgonjwa, watakuwa wanashauriwa kutafuta matibabu zaidi ikibidi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya maradhi ya figo kutokana na ukosefu wa kituo cha matibabu ya figo nchini Tanzania. Gharama ya kusafirisha wagonjwa wa hali hii nje ya nchi si tu ghali kwa serikali bali hata kwa wagonjwa wenyewe hukosa fedha za kutosha kuwawezesha kupata tiba bora nje ya nchi. Hivyo kliniki hii ya siku mbili kupitia madokta hawa ni baraka kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na figo na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo  ambao hawawezi kumudu kusafiri nje ya nchi kwa matibabu zaidi.
Bw. Radhey Mohan, Makamu Rais  wa Shirika la kimataifa la Maendeleo ya Biashara ndiye anayewezesha kliniki hiyo katika hospitali Hindu Mandal.

Related

OTHER NEWS 8808126485158008423

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item