KENYA AIRWAYS YATANGAZA HASARA KUBWA

Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) limetangaza hasara kubwa ya Shilingi bilioni 25.7 za Kenya sawa na dola milioni 2.57 katika ki...



Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) limetangaza hasara kubwa ya Shilingi bilioni 25.7 za Kenya sawa na dola milioni 2.57 katika kipindi cha fedha cha mwaka wa 2014-2015.
Hii ni hasara ya asilimia 661% ikilinganishwa na kipindi cha fedha cha mwaka wa 2013-2014.
Mwaka uliopita kampuni hiyo ya ndege ilitangaza kuwa imepata hasara kubwa wakati huo ya shilingi bilioni 3.3 mwaka uliopita wa kifedha.
Uongozi wa shirika hilo unasema kuwa hasara hii kubwa imetokana na kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya Kenya.
Shilingi ya Kenya imeporomoka kwa asilimia 11 ya thamani yake katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita miongoni mwa sababu zingine.
''Ushindani kutoka kwa mashirika ya ndege kutoka ghuba na mashariki ya kati, mbali na swala kuu la ugaidi imechangia pakubwa hasara kubwa tuliyopata ''alisema Mkurugenzi mkuu mtendaji Mr. Mbuvi Ngunze.

Bwana Ngunze ambaye amechukua wadhfa huo mwezi Desemba mwaka uliopita kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa kipindi kirefu Dr. Titus Naikuni, anasema kuwa Kenya Airways imekumbwa na msukosuko wa masoko yake kwani yaliathirika na ugonjwa wa Ebola kwa kipindi kirefu cha mwaka uliopita, na mfumuko wa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Habari hii sio nzuri kwa wenye hisa wakuu ambao ni Serikali ya Kenya ambayo tayari, ilikuwa imeipa shirika hilo la KQ mkopo zaidi wa shilingi bilioni 4.2 za Kenya ilikuisaidia kurejesha ushindani wake na kuiwezesha kulipa mishahara wafanyikazi wake.
Kulingana na shirika hilo kurejea kwao katika soko lake la Magharibi mwa Afrika kutaiwezesha kuleta faida tena.
KQ vilevile iko mbioni kutafuta mkopo zaidi wa dola milioni 200m kutoka kwa benki ya Afrexim ilikuiwezesha kutekeleza wajibu wake kabla ya kutathmini kima cha madeni yake.


Related

TUJUZANE 534016653550878077

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item