MAJAMBAZI WATANO WANAODAIWA KUWAPIGA RISASI ASKARI POLISI KITUO CHA POLISI CHA SITAKISHARI WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM
Jeshi la polisi nchini Tanzania limetangaza kupata mafanikio makubwa katika operation maalum inayoendelea ya kuwasaka watu waliohusik...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2015/07/majambazi-watano-wanaodaiwa-kuwapiga.html
Jeshi la polisi nchini Tanzania limetangaza kupata mafanikio makubwa katika operation maalum inayoendelea ya kuwasaka watu waliohusika katika shambulio la kuvamia kituo cha polisi cha stakshari jijini Dar es salaam na kuendesha mauaji ya askari wanne wa kituo hicho pamoja na raia waliokua katika kituo hicho huku wakipora kiasi kikubwa cha silaha na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza na wanahabari muda jijini Dare s salaam kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA amesema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wema wamefanukiwa kukamata bunduki 16 huku 14 zikiwa ni zile zilizoibiwa katika tukio la kituo cha staki shari na mbili zikiwa bado hazijulikani ziliporwa kwa watu gani,
Amesema kuwa zoezi la kuwasaka watuhumiwa hao lilianza mara baada ya kutokea kwa tukio la stakishari ambapo ilipofika tarehe 17 mwezi huu majambazi hao walijipanga kufanya tukio myinginme maeneo ya mbagala jijini Dar es salaam ambapo wananchi walitoa taarifa kwa jeshi la polisi na wakajipanga tayari kuwakabili.
Sanduku lililokua limehifadhi pesa taslimu million 170 na kufukiwa chini huko mkuranga
Amesema kuwa baada ya kufika eneo la Twangoma mbagala polisi walijipanga kuwakabili na baadae majambazi hao walitokea na kuanza kushambuliana na askari hao ambapo katika mapamano hayo majambazi watano walikamatwa ambapo watatu kati yao walikuwa tayari wameshakufa na wawili wapo hai hadi leo
Katika taarifa nyingine ambazo jeshi la polisi kanda maalum ya dar es salaam walizipata juzi tarehe 19 ni kuwa kulikuwa na taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna tetesi kuwa silaha zilizoibiwa kituo cha stakishari zilikuwa zimefichwa katika maeneo ya Mkuranga.
Jeshi la polisi waliweka kambi katika maeneo hayo na kuanza msako maalum wa kuzisaka mahali ambapo silaha hizo zilikuwa zimefichwa ambapo katika tukio la kushangaza lilionekana eneo ambalo lilikuwa limewekwa kinyesi cha binadamu na polisi kupatilia mashaka na ndipo walipoamua kupachimba na kufanikiwa kupata silaha hizo.
Baada ya kuchimba maeneo hayo jeshi la polisi lilifanikiwa kukuta silaha aina ambazo ni bunduku aina ya 16 ambazo 14 ni za stakishari,na risasi 55 huku risasi 28 ni zile zilizoibiwa katika tukio la Stakishari.
Pamoja na silaha hizo jeshi hilo lilikuta sanduku kubwa lililokuwa na hela kiasi cha shilingi million sabini ambazo hazikujulikana mara moja zilikuwa na lengo gani huku KOVA akisema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.
Aidha kamishna kova amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo yaliyopatikana katika operation hiyo bado jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linaendelea na kazi kubwa ya kuwasaka wahalifu hao kwa kuwa bado kuna silaha nyingi ambazo ziliporwa katika tukio la stakishari na bado hazijapatikana.