SMZ YAZUIA KIWANJA CHA WATOTO KUTUMIKA SIKUKUU ZA IDD EL FITR

Na Rahma Suleiman   Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kiwanja cha kufurahisha watoto kilichopo eneo la Kariakoo, mjini...


Na Rahma Suleiman
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kiwanja cha kufurahisha watoto kilichopo eneo la Kariakoo, mjini Unguja, hakitatumika katika Sikukuu ya Idd El Fitr, mwaka huu, kutokana na ujenzi wake kutokamilika.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kukagua kiwanja hicho, Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee, alisema dhamira ya serikali ni kuona kiwanja kinakamilia mapema lakini kumejitokeza changamoto za kiufundi.

Alisema pamoja na bembea zote 12 kukamilika, baadhi ya maeneo yanaendelea kufanyiwa matengenezo, ambayo yatachukua zaidi ya miezi miwili kukamilika kwake.

Mzee alisema hata kama kiwanja hicho kitafunguliwa kwa muda kwa ajili ya sikukuu inayoanza mwanzoni mwa wiki ijayo, kutakuwa na wasiwasi wa usalama, kwani hata milango mikuu haijawekwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) inayowekeza katika mradi huo, Khamis Filfil Thani, alisema matumaini yake kuwa ifikapo Sikukuu ya Idd El Hajj, mwaka huu, kiwanja hicho kitakuwa tayari kutumika.


Hali hiyo pia iko katika kiwanja kama hicho kilichoko Tibirinzi, Chake Chake, Pemba, ambako kazi ya matengenezo yaliyotarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu, yatachukua wiki mbili kutoka sasa.

Serikali ililazimika kuvifanyia matengenezo viwanja hivyo kutokana na uchakavu wa bembea, kwani zilikuwa zinahatarisha usalama wa watoto.

 
CHANZO: NIPASHE

Related

TUJUZANE 984601004499925669

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item