KCB BENKI YATOA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI KIIMBWA MKURANGA

  walimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kiimbwa iliyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Eugema Njau(kushoto) akipokea moja ya msaada wa madawa...

 walimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kiimbwa iliyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Eugema Njau(kushoto) akipokea moja ya msaada wa madawati kati ya  100 toka kwa Ofisa Masoko wa Benki ya KCB Tanzania, Margaret Mhina (kulia) Msaada huo ni mwendelezo wa mradi wao wa kugawa  madawati 1000 kwa shule za msingi. Wanaoshuhudia wapili kutoka kushoto ni  Mwenyekiti wa kijiji Ramadhani Bakari na Meneja wa benki hiyo  tawi la Buguruni Luck Mwakitalu.

 Ofisa wa Benki ya KCB Tanzania,Magret Mhina(kushoto)akimsalimia Kwega Athumani(10) ambaye ni mwanafunzi mlemavu wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kiimbwa ya Mkuranga mkoa wa Pwani,Wakati alipotembelea shuleni hapo kukabidhi msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na benki yake.Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo.

 Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiimbwa iliyopo Mkuranga Mkoa wa Pwani wakimsikiliza kwa makini Meneja wa benki ya KCB Tanzania tawi la Buguruni, Luck Mwakitalu wakati wa hafla ya kukabidhiwa  msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na benki hiyo ikiwa ni mwendelezo wa mradi wao wa kugawa madawati 1000 kwa shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

 Ofisa Masoko wa Benki ya KCB Tanzania, Margaret Mhina(kushoto) akimkabidhi moja ya madawati kati ya 100 Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Kiimbwa iliyopo wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,Ramadhani Bakari kwa niaba ya shule hiyo iliyonufaika na msaada wa madawati hayo ikiwa ni mwendelezo wa mradi wa benki hiyo katika kutoa msaada wa madawati 1000 kwa shule za msingi(10)za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.Wengine katika picha wapili toka  kushoto waliokaa ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo  Eugema Njau na Meneja wa benki hiyo tawi la Buguruni,Luck Mwakitalu. 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kiimbwa iliyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,wakiwa wamekalia madawati mapya 100 waliyopatiwa msaada na Benki ya KCB Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa mradi wao wa kugawa madawati 1000 katika shule za msingi(10) za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Related

ELIMU 2760109772075903172

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item