WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AWAWEKA MATATANI VIONGOZI WA MKOA WA KIGOMA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa NSSF katika kikao cha majumuisho y...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2015/12/waziri-mkuu-mh-kassim-majaliwa-awaweka.html
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa NSSF katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku mbili mkoani humo Desemba 30, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, mkoani Kigoma imewaacha matatani baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, baada ya kubaini uuzwaji wa majengo ya halmashauri kinyume na taratibu.
Majengo hayo ni pamoja na jengo la Kigodeco, Jengo lilokuwa likitumiwa na Miboss, Jengo la Mwanga Center, viwanja 16 pamoja na msitu wa Masanga, hali hiyo iliyopelekea Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kutoa agizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Mhandisi John Ndunguru kusimamia mchakato wa ufuatiliaji wa tuhuma hizo mpaka itakapofika Januari 2, 2016 ambapo atatakiwa kuwasilisha ripoti katika ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo hii jana kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku tatu mkoani humo katika ukumbi wa NSSF, ambapo alisema kuwa uchunguzi unaonyesha uuzwaji wa mali hizo za umma haukuwa wa kihalali.
Awali uzwaji wa majengo ulisitishwa na uongozi wa mkoa kwa kuwa mali hizo ni sehemu ya mali ya umma, lakini licha ya kusitishwa huko Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Boniface Nyambele kwa kushirikiana na madiwani wa Halmashauri hiyo waliuza mali hizo.
“Leo Mkurugenzi na Mhandisi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mtaenda kwa Katibu Tawala wa Mkoa na kutoa maelezo kwa maandishi kuhusu mchakato mzima wa uuzwaji wa majengo na viwanja hivyo kwa bei ya kutupa,” ameagiza Waziri Mkuu.
Aidha baadhi ya madiwani walikuwa katika mchakato huo Asha Omari na Mgeni Kakolwa kwa nyakati tofauti wamekiri majengo kuuzwa kwa utashi wa Mkurugenzi wa Halmashauri akishirikiana na aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyo Bakari Beji na Naibu wake Rashidi Ruhomvya.
“Mwezi wa saba tuliitwa katika kikao cha dharura lakini ajenda za kikao hatukuzifahamu, baada ya kuingia tukakuta ajenda ya kuuzwa kwa mali hizo, tulivutana baina ya madiwani wa CCM na CHADEMA, lakini kwakuwa madiwani wa CCM tulikuwa wachache ajenda hiyo ilipitishwa na kuuzwa kwa mali hizo za umma” wamebainisha Madiwani hao.
Kwa mujibu wa madiwao hao, jengo la Kigodeco liliuzwa kwa kiasi cha shilingi milioni 375 ambapo katika fedha hizo,kiasi cha cha milioni 167 zirirudishwa kwa mzabuni aliyekuwa amekodisha jengo hilo baada ya kukatisha mkataba na sh.milioni 100 walidai wanawekeza katika ujenzi wa maabara wa shule za skondari za manispaa hiyo.
Wakati huohuo kiongozi mmoja wa manispaa hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema, uvumi huo unahusisha watu wengi kwa kuwa mkurugenzi hawezi kuuza bila kushirikiana na wenzake ambao walianzisha mchakato huo na shida kubwa ni kutokana na utashi wa siasa.