MKUTANO MKUU WA UEFA KUFANYIKA TAREHE 24 MAY 2013

Mkutano mkuu wa UEFA unaoshirikisha nchi wanachama 53 umepangwa kufanyika  huko jijini London siku ya ijumaa ya tarehe 24/05/2013 na ag...


Mkutano mkuu wa UEFA unaoshirikisha nchi wanachama 53 umepangwa kufanyika  huko jijini London siku ya ijumaa ya tarehe 24/05/2013 na agenda za mkutano huo zimekwisha tolewa. Mkutano huu wa 37 unategemewa kufanyika katika hoteli ya Grosvenor House, Park Lane huko London.

Nchi 53 wanachama wa UEFA hukutana kila mwaka, na kwa mwaka huu ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na:
  1. Ripoti ya mwaka ya rais wa UEFA na kamati kuu na ripoti ya kiutawala ya UEFA kwa mwaka 2011/2012
  2. Ripori ya kazi za kamati za UEFA
  3. Maswala ya fedha yakihusisha bajeti kwa mwaka 2013/2014
  4. Uchaguzi wa kamati kuu
  5. Swala la ubaguzi wa rangi kwa soka la ulaya
  6. Maombi ya uanachama wa  chama cha mpira wa miguu cha Gibraltar kwa UEFA
kamati kuu ya UEFA inategemewa kukutana tarehe 22 na 23 mwezi huo wa tano kabla ya mkutano mkuu.

SOURCE: UEFA website

Related

NEWS ALERT! MSIGWA AACHIWA

Mahakama Iringa imemuachia kwa dhamana Mch. Peter msigwa baada ya kusomewa mashitaka yake hivi punde na kukana shitaka la kujeruhi, kesi imeahirishwa na kutarajiwa kutajwa tena Machi 10, 2013.

MSIGWA AFIKISHWA MAHAKANI LEO

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mh. Peter Msigwa amefikishwa mahakamani asubuhi hii akihusishwa na vurugu zilizotokea jana jioni akihusishwa na uchochezi wakati wa kampeni za udiwani kata ya Nduli....

IGP MANGU AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI

IGP ERNEST MANGU INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, amepangua baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa, wapelelezi na wakuu wa polisi wa usalama barabarani, pamoja na watendaji wen...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904819
item