NDUGAI ASHTAKIWA KWA WAPIGA KURA WAKE

  MBUNGE wa Jimbo la Ubungo na Kiongozi wa Kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amemshitaki Naibu Spika wa B...

 
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo na Kiongozi wa Kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amemshitaki Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai kwa wapiga kura wake, akiwahoji iwapo walimtuma bungeni kufanya Ubabe wa  kuwatoa nje wabunge wenzie badala ya kuwatetea.
Mnyika alitoa Mashitaka hayo jana Aprilli 26, 2013 katika kijiji cha Iyegu, Kata ya Mlali, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, ambapo alisema amemkatia Rufaa Ndugai mara Tano bungeni bila majibu, kwa hiyo jana aliamua kumshitaki kwao ili wafanye maamuzi magumu juu ya mbunge wao asiyefanya kazi waliyomtuma.
Akizungumza katika Mkutano huo Mnyika alimshitaki Ndugai akiwahoji kama walimtuma kufanya hivyo, na waliposema Laa, aliwataka kufanya mabadiliko ya mwakilishi wa Jimbo lao kama wanataka kumaliziwa Kero zao zikiwepo Haki na Maendeleo ya kiuchumi na Matumizi bora ya Rasilimali zao.
Mwananchi mmoja alimhoji Mnyika “Je, ni nani aliyetayarisha, kulinda, kusimamia na kusafirisha Twiga wetu kwenda nje, lini watarejeshwa na waliohusika watafanywaje?.
Mnyika aliwajibu wananchi kwamba, wahusika wa usafirishaji wa Twiga wao ni vigogo walioko madarakani, na Twiga hao wako nchi mmoja ya Kiarabu, na mbali ya Twiga hao hivi karibuni Chadema itaibua suala la Tembo, na kuwaambia suluhisho la haraka kwa yote hayo ni kufanya mabadiliko ya viongozi mafisadi haraka.
Alipoulizwa Mauaji na Vitisho wanavyofanyiwa na Kundi linalojiita Kanyaga Twende, wanapoamua kujiunga na  vyama Upinzani, Mnyika aliwauliza kama wanayo simu ya Mbunge wao wamuulize ila wasimtukane, na waliposema hawana aliwatajia namba ya Ndugai na ya Mkurugenzi wa Usalama Chadema ambaye alidai atawawasaidia dhidi ya vitisho .
Aidha Mnyika kabla ya kushuka Jukwani saa 11.30 jioni, aliuuliza umati uliokuwepo uwanjani hapo, wangapi wapo tayari kwa mabadiliko ya M4C, watu wote karibu 1,000 walinyosha mikono na Mnyika akashuka kuelekea Kongwa kuungana na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, kuendelea na Mikutano mingine.
SOURCE: CHADEMA BLOG

Related

MNYIKA ASHINIKIZA KUPATA HATI YA MUUNGANO

  Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, John Mnyika, amesema atawasilisha hoja kuzuia shughuli za Bunge hilo kuendelea mpaka wajumbe watakapopatiwa hati halisi ya Muungano.Mnyika, ambaye ni ...

BUNGE MAALUM LAANZA KUSIKILIZA TAARIFA ZA KAMATI

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta amesema mjadala kuhusu  taarifa za Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu  ya  Katiba  ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanza...

TAARIFA YA MBEYA CITY KUHUSU TUHUMA ZA KUPEWA RUSHWA NA AZAM ILI WAFUNGWE KWENYE MECHI YAO

TAARIFA KWA UMMA UPOTOSHAJI UNAOTOLEWA DHIDI YA TIMU YETU KUELEKEA MCHEZO WA TAREHE 13/4/2014 Kwanza nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo wa mpira wa miguu na wa...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904819
item