CUF YAKANA KUHUSIKA NA VURUGU ZA MTWARA

  DAR ES SALAAM.  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimekana kuhusika na vurugu zinazotokea katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na kwamba zinatokana n...


 DAR ES SALAAM. 
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimekana kuhusika na vurugu zinazotokea katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na kwamba zinatokana na sera mbaya za Serikali za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alisema wamepata taarifa kuwa katika vikao vya viongozi wa mikoa hiyo, wamekuwa wakiishutumu CUF kuwa ndiyo inayosababisha vurugu hizo.
“CUF haiungi mkono vurugu, tunataka wananchi wadai haki zao kwa njia ya amani lakini inapotokea wananchi wakafanya vurugu Serikali iwajibike kwani yenyewe ndiyo imezuia haki za wananchi,” alisema Mtatiro.
Alisema mfumo wa stakabadhi ghalani katika ununuzi wa korosho na gesi ni mambo yanayowafanya wananchi wa mikoa hiyo kusababisha vurugu.
Mtatiro alisema kwa mfano zao la korosho, wakulima wamekuwa wakidhulumiwa kwa kutokulipwa fedha za awamu ya pili kwa kisingizio cha kushuka kwa bei ya zao hilo katika soko la dunia.
“ Kilo moja ya korosho inauzwa kwa Sh1,200 kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, awamu ya kwanza hulipwa Sh600 lakini awamu ya pili wamekuwa hawalipwi ama wakati mwingine wanalipwa Sh200, zinazobaki Sh400 zinakwenda wapi, ndiyo maana wananchi hawa wanafanya vurugu,” alisema.
Alisema wananchi wa Lindi na Mtwara wanafahamu haki zao na kuzidai.
“CUF inaionya Serikali ya CCM isitafute mahali pa kubambikizia makosa, viongozi wa CUF wasiendelee kugeuzwa kuwa ndiyo wa kuhojiwa kuhusu makosa ya Serikali na CCM,” alisema Mtatiro katika taarifa yake.
Alisema Serikali inapaswa kuwahoji watendaji wake na sera zake mbovu, ilizoshindwa kuongoza nchi.
Kwa mujibu wa CUF, wabunge kadhaa wa Mikoa ya Lindi na Mtwara walihojiwa katika vikao hivyo wakidaiwa kuwa ni miongoni mwa watu wanaopandikiza chuki kwa wananchi.    
 
Source: Mwananchi

Related

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA KUHUSU MITAALA KWA VYUO VYA KIISLAM, MOROGORO

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana wakati akiwasili katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa...

DAKTARI FEKI AMEKAMATWA MANYARA AKIDAI NI DAKTARI WA MAGONJWA YA MOYO

  Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa ya mkoani Manyara kwa kushirikiana na polisi wamefanikiwa kumnasa mkazi wa jijini Dar-es-salaam Bw Godlove Sozigwa akituhumiwa kuomba kufanya...

MANISPAA YA KINONDONI YAFANYA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM JIMBO LA KAWE

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa kwenye Jengo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) ambalo linajengwa katika eneo la Mabwepande, likiwa ni sehemu ya Ho...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904822

HOT POSTSRECENTArchive

RECENT

Archive

item