Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini wakati wa kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/05/kikao-cha-mwenyekiti-wa-ccm-rais.html
|
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini wakati wa kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Spika wa Bunge Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula |
|
Wabunge wa CCM |
|
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib kwenye kikao hicho. |
|
Mbunge wa Songea na Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akitaniana kuhusu Uyanga na Simba na Mwenyekiti wa Simba, Mbunge wa Tabora Aden Rage nje ya ukumbi kabla ya kuanza mkutano huo. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya. |
|
Mbunge wa Bunga Steven Wasira (kulia) akibadulishana mawazo na wabunge wenzake, Dk. Kamani na Mkullo kabla ya kikao kuanza |
|
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan (kushoto) akibadilishana mawazo na wabunge wenzake Khamis Kagasheki na Shabiby nje ya ukumbi |
|
Shabiby akizungumza na Angela Kairuki |
|
Vicky Kamata na Ana Kilango Malecela ukumbini |
|
Dk. Asha-Rose Migiro akimsalimia Mama Anna Kilango Malecela |
|
Dk Maua Daftari na Samiah Suluhu ukumbini |
|
Job Ndugai akimpongeza Mbunge wa Igunga Dk. Dalaly Peter Kafumu kurejeshewa Ubunge |
|
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimsalimia Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa wakati wa kikao hicho cha Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na wabunge wa CCM |
|
Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini Mbunge mwenzake Innocent Kalogeris wakati wa mkutano huo. Picha zote na BASHIR NKOROMO |
Picture thanx to CCM social Media