VIINGILIO VYA MECHI KATI YA TAIFA STARS NA IVORY COAST HIVI HAPA

Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) itakayoch...


Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku mbili kabla ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.

VitiBei ya tiketiIdadi ya watazamaji
Kijani5,00019,648
Rangi ya bluu7,00017,045
Rangi ya chungwa10,00011,897
VIP C15,0004,060
VIP B20,0004,160
VIP A30,000748

Twende kuishangalia timu yetu, utaifa kwanza.

Related

OTHER NEWS 3106482086631968853

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item