HII NDIO RATIBA KAMILI YA RAIS BARACK OBAMA ILIYOTOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili. Katika Uwan...


Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Obama ambaye atafuatana na Mkewe Mama Michelle atapokelewa na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Baada ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete. Aidha, atafanya mkutano na Wafanyabiashara na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.

Tarehe 2 Julai 2013, Mhe. Rais Obama atatembelea Mitambo ya kufua Umeme ya Symbion iliyopo Ubungo, Dar es Salaam na kuzindua rasmi Mpango Maalum wa Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na Marekani (Power Africa Initiative).

Mpango huo utaanza na nchi saba ambazo ni: - Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Sudan Kusini.

Mhe. Rais Obama anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 02 Julai 2013.


IMETOLEWA NA:
 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, 
DAR ES SALAAM
30 JUNI, 2013 0 MAONI

Related

TCRA YATOA ONYO KWA WANAOTUMIA MITANDAO KUCHAFUA WENGINE

Dr. Raynold Mtungahema Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA, imewaonya wale wote wanaotumia mitando kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo watakabiliwa na mkono wa sheria....

AJINYONGA KWA KUKOSA KODI YA CHUMBA

Marehemu Geofrey Ndibalema (41), mkazi wa Tandika jijini Dar aliyejinyonga kwa kukosa kodi ya chumba   INASIKITISHA! Geofrey Ndibalema (41), mkazi wa Tandika jijini Dar amedaiwa kujin...

SEHEMU YA UBUNGO MATAA KUFUNGWA KUPISHA UJENZI WA BARABARA

  KAMPUNI ya ujenzi ya Strabag  inayojenga barabara ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) imetangaza mabadiliko ya muda katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam kuanzia kesho na...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item