RAIS MSTAAFU WA MAREKANI GEORGE W. BUSH NA MKEWE LAURA KUKUTANA NA RAIS BARACK OBAMA KESHO

RAIS mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura wanatarajiwa kesho kuwa nchini kuhutubia kongamano linalojadili wajibu wa wake wa...


RAIS mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura wanatarajiwa kesho kuwa nchini kuhutubia kongamano linalojadili wajibu wa wake wa marais katika kuinua wanawake duniani.

Kuwasili kwa Bush, ni mwendelezo wa wiki hii Jiji la Dar es Salaam kuwa katika pilikapilika za kupokea ugeni wa watu maarufu. Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya George Bush na litafanyika kesho na keshokutwa.

Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari , inasema kongamano hilo litahudhuriwa na wake mbalimbali wa marais akiwemo mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama.

Pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair atahudhuria. Wake wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji), Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia.


Kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili masuala ya kuwekeza kwa wake, kuimarisha Afrika lakini pia wajibu wa wake wa marais katika kuhamasisha wanawake katika maeneo ya elimu, afya na kuwakwamua kiuchumi.


“Kongamano hili litawakutanisha pamoja wake wa marais kutoka nchi mbalimbali duniani, maofisa wa Serikali, mashirika binafsi, Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) na wasomi kwa ajili ya kujadili mambo muhimu ya kuchukuliwa hatua ili kuweza kuwanufaisha wanawake,” ilisema taarifa hiyo.




Aidha mada zitakazowasilishwa na kujadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na kuinua wajasiriamali wanawake kiuchumi kupitia mafunzo na teknolojia, kuwapatia fursa wanawake wakulima kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa, mafunzo kuhusu saratani ya matiti na umuhimu wa elimu kwa wanawake.


Amani, utulivu na uimara wa mfumo wa demokrasia ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuvutia viongozi hao wa kimataifa kuja nchini

Related

KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM ZANZIBAR LEO

 Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Ka...

NDESAMBURO AMKINGIA KIFUA LOWASA

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionekana kutikiswa na ushawishi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wa kutaka kutimiza safari yake ya kuwapatia Watanzania elimu bure, Mbunge wa Mosh...

WAFUGAJI, WAKULIMA VITANI KITETO

MZAHA na uzembe unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wilayani Kiteto na mkoani Manyara katika kusuluhisha mgogoro wa wafugaji na wakulima, umesababisha mauaji ya watu zaidi ya 13 usiku wa ku...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item