IFAHAMU METHADONE-TIBA TEGEMEZI KWA WATUMIA DAWA ZA KULEVYA
Methadone ni dawa inayotumika kutibu utegemezi wa dawa zingine za kulevya mfano; heroin,codeine,pethine na morphine. Dawa ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/08/ifahamu-methadone-tiba-tegemezi-kwa.html
Methadone ni dawa inayotumika kutibu utegemezi wa dawa
zingine za kulevya mfano; heroin,codeine,pethine na morphine.
Dawa hii hutolewa kwa kipimo maalum chini ya usimamizi wa
mtaalamu.Hivyo hupunguza maambukizi ya VVU na Homa ya Ini [B na C] kwa
wanaojiunga.Hapa Tanzania,kwa sasa huduma hii inatolewa na hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Tiba ya methadone huzuia ‘arosto’ na kupunguza au kuondoa utegemezi wa dawa za kulevya.
Jibu:Hapana.
Kwanza
kabisa matumizi ya methadone hutolewa kama tiba na kupewa kwa wale wenye
utegemezi wa dawa za kulevya.
Kwa wagonjwa
wa namna hii kwao ni mbadala salama wa dawa za kulevya wanazotumia kama vile
heroin.
Inawaweka
huru kutoka kwenye kulazimika kutafuta dawa za kulevya na kuwapa fursa ya
kuboresha maisha yao.
Je,utajisikiaje ukitumia methadone?
Watu
wakianza kutumia tiba ya methadone,baadhi hujisikia raha iliyozidi na kujisikia
kusinzia hali ambayo pia huletwa na baadhi ya dawa nyingine za kulevya.
Je,unaweza kutumia methadone na dawa
zingine?
Methadone ni
dawa yenye nguvu sana na inaweza kuwa na mwingiliano na dawa nyingine na kuleta
madhara.
Mweleze
daktari au mfamasia kuhusu dawa ulizo kunywa kabla ya kutumia methadone.
Ni muhimu
kumweleza mfamasia au daktari kama umekunywa pombe au dawa ya usingizi kwa
mfano valium,fenegani au piriton maana huweza kuleta kifo kama itanywewa pamoja
na Methadone.
Kuchanganya
dawa ya methadone na dawa nyingine za kulevya kunaweza kusababisha mwili
kuzidiwa na dawa(overdose),hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha.