KIKAO CHA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI CHASHINDWA KUFANYIKA

Mbunge Peter Mathuki kutoka Kenya aliyewasilisha hoja binafsi kwenye bunge la EAC jana   Sakata la vikao vya Bunge la Afrika Mashari...

Mbunge Peter Mathuki kutoka Kenya aliyewasilisha hoja binafsi kwenye bunge la EAC jana
 
Sakata la vikao vya Bunge la Afrika Mashariki kufanyika kwenye nchi wanachama kwa mzunguko limeingia katika sura mpya baada ya kikao  cha leo jioni kuvunjika kufuatia Spika wa Bunge hilo,Magreth Zziwa Nantongo kukataa hoja binafsi ya mbunge kutoka Kenya Peter Mathuki aliyetaka utaratibu wa zamani kufanya vikao kwenda nchi wanachama uendelee.
Mbunge alimama na kuomba kuwasilisha hoja hiyo ambayo Spika aliitupilia mbali kuwa haina mashiko na kusababisha wabunge kutoka Rwanda kutoka nje ukumbi wa bunge yalipo makao makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.
Spika alitoa mapumziko na mashauriano ya dakika 15 na aliporejea wabunge wapatao 14 tu ndio walikubali kuingia ukumbini huku wengine wakigomea uamuzi wa Spika kukataa hoja ya mbunge kuwasilishwa na kuamua kuahirisha bunge hadi kesho.
Wabunge wanaounga mkono vikao kufanyika Arusha wanadai kuwa ni jambo la busara kutokana na kuwa ndio makao makuu ya EAC na fedha nyingi zimetumika kujenga makao hayo na iwapo vikao vya bunge vitafanyika kwa kuzunguka nchi wanachama zitatumika fedha nyingi kulipia kumbi za kufanyia vikao hivyo fedha ambazo zingetumika kwa shughuli za maendeleo.
Kwa upande mwingine wanaotaka vikao vya bunge vifanyike kwa mzunguko wanajenga hoja kuwa itasaidia kujenga uelewela wa mtangamano kwa wananchi na taasisi za kiraia kufatilia mwenendo huo kwa karibu.
Mbunge wa Tanzania,Nderakindo Kessy alipotakiwa kutoa maoni yake alisema jambo hilo limechukua sura mbaya na anayeweza kulizungumzia ni Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Adam Kimbisa ambaye hakuwepo na alipotafutwa Katibu wake Shyrose Bhanji alikua kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi.

Related

TAMKO LANGU KWA UMMA KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ndugu wanahabari na wa Tanzania wenzangu, Nimekuwa nikilazimika kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanahabari, ndugu, jamaa na marafiki kuhusiana na namna mchakato wa kuandika katiba mpya y...

GRACE MVANDA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA IRINGA

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempitisha Grace Tendeya Mvanda, kuwa mgombea wake katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo la Kalenga, mkoani Iringa. Grace M...

VIBER MESSAGING APP BOUGHT BY JAPAN'S RAKUTEN

Messaging app Viber has been bought by Rakuten, the owner of online retailer Play.com. The Japanese company will pay $900m (£540m) for the mobile application, which offers free calls and text ...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item