TAMKO LA UMOJA WA WANAZUONI KUHUSU TUKIO LA SHEIKH PONDA

Sheikh Suleiman Amran Kilemile TAMKO LA UMOJA WA WANAZUONI WA KIISLAMU TANZANIA KUHUSU TUKIO LA SHEIKH PONDA Sisi, Umoja wa...

Sheikh Suleiman Amran Kilemile
TAMKO LA UMOJA WA WANAZUONI WA KIISLAMU TANZANIA KUHUSU TUKIO LA SHEIKH PONDA

Sisi, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay – atul Ulamaa), tumepokea kwa masikitiko makubwa habari za kushambuliwa na kujeruhiwa kwa silaha za moto, Sheikh Ponda Isa Ponda, huko Morogoro, Jumamosi Agosti 10, 2013.

Hay-atul Ulamaa, imesitushwa na tukio hili linalo uma na linaloumiza na kuleta mshtuko na fazaa katika jamii kama ilivyoshtushwa na matukio mengine kama hili hapa nchini. Hili ni tukio ambalo linaashiria kuwa walio litenda hawaitakii mema na amani nchi yetu.

Tunalaani vikali kitendo hicho na tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua kali na za haraka dhidi ya wale wote walio husika katika tukio hili lenye kuumiza nyoyo za wengi.

Aidha tunawasihi Waislamu na jamii kwa ujumla kuwa watulivu, wenye subira na wenye kunyenyekea kwa Mola wao katika jambo hili zito, wakati tunasubiri vyombo vya dola vichukue hatua zinazo stahiki dhidi ya wahusika wa tukio hili.

Tunamuombea Sheikh Ponda Isa Ponda Allah Amponye haraka na Am,pe baraka katika umri wake. Amin

Sheikh Suleiman Amran Kilemile

Mwenyekiti

Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania.
11/August/2013
 

Related

MABILIONI YA USWIS YAHAMISHWA KIMYAKIMYA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema   Mabilioni ya shilingi yaliyowekwa na Watanzania katika benki za Uswisi yameanza kuhamishwa kimyakimya. Ripoti ya Benki za Uswisi ya 20...

RAIS KIKWETE APOKEA RIPOTI YA MGAWANYIKO WA WATU KWA UMRI NA JINSI IKULU, DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho Ripoti ya Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia kwa data za sensa ya watu na makazi mwaka 2012 ...

SITTA ALIPOCHUKUA FOMU KUWANIA UENYEKITI BUNGE LA KATIBA

 Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akipokea Fomu kutoka kwa Ofisa wa Bunge Bi. Lidya Mwaipyana Katikati ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Nzega Hamisi...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904824

HOT POSTSRECENTArchive

RECENT

Archive

item