WAASI WA M23 KUSITISHA MAPIGANO DRC
Waasi wa M23 Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema kuwa watasitisha mapigano, kufuatia makabiliano makali na wanaje...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/08/waasi-wa-m23-kusitisha-mapigano-drc.html
Waasi wa M23 Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Congo wamesema kuwa watasitisha mapigano, kufuatia makabiliano makali
na wanajeshi wa serikali wanaoungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa
Mataifa.
Afisa mmoja wa Kundi hilo la M23 Museveni
Sendugo, ameiambia BBC kuwa wanajeshi wake tayari wamerudi nyuma umbali
wa kilomita tano kutoka eneo la mapigano.
Kiongozi
wa kundi hilo Bertrand Bisima amesema uamuzi huo utaruhusu wachunguzi
huru kupeleleza jinsi makombora yalivyorushwa nchini Rwanda siku ya
Alhamisi.
Serikali ya Rwanda imesema jeshi la Congo lilirusha makombora hayo, madai ambayo yamekanusha na serikali ya Congo.
Wengi wa wapiganaji wa M23 ni wanajeshi walioasi
jeshi la serikali, wengi wao wakiwa wa kibila la Kitutsi sawa na
uongozi wa Rwanda.
Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeishutumu
serikali ya Rwanda kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa kundi hilo la M23,
tuhuma ambazo zimekanushwa na utawala wa Kigali.
Awali, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa
rais wa Rwanda, kuwa mvumilivu huku uhasama kati yake na nchi jirani ya
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ukiendelea kutokota katika maeneo ya
mipakani.
Bwana Ban, alizungumza na rais Paul Kagame baada
ya serikali yake kuishutumu Congo, kwa kufanya shambulio katika ardhi
yake makusudi na kumuua mama mmoja na kumjeruhi mtoto wake.
Msaidizi wa katibu huyo mkuu wa Umoja wa
Mataifa, amenukuliwa akiiambia Umoja wa Mataifa kuwa wapiganaji wa kundi
la waasi wa M23, wameonekana wakirusha makombora wakilenga Rwanda.
Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeshutumu
Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao wa M23, madai ambayo yamepingwa
vikali ya utawala wa Kigali.
Wanajeshi wa Congo wakishirikiana na wanajeshi
wa Umoja wa Mataifa, wamekuwa wakifanya mashambulio dhidi ya waasi hao
wa M23 karibu na mpaka wa Rwanda, tangu wiki iliyopita.
Waasi walengwa na UN
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kutunza amani
nchini DRC, Monusco, kiliimarishwa zaidi pale wanajeshi elfu tatu zaidi
walipotumwa nchini humo kupambana na waasi hao.
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise
Mushikiwabo, amesema mabomu na makombora kumi na tatu yalirushwa katika
ardhi yake siku ya Jumatano na mengine kumi siku ya Alhamisi.
Waziri huyo amedai kuwa kufikia sasa wanajeshi hao wa Congo wamefanya mashambulio thelathini na nne nchini Rwanda.
Amewashutumu wanajeshi wa DRC kwa kuwalenga raia
wake na kusisitiza kuwa kwa sasa wanajiepusha kulipisa kisasi lakini
hawatasita kujibu ikiwa uchokozi huo hautakoma.
Msemaji wa jeshi la Congo Kanali Olivier Hamuli
ameiambia BBC kuwa jeshi lake haliwezi kurusha makombora kulenga maeneo
yanayokaliwa na raia.
''Waasi ndio wanaoweza kufanya kitendo kama
hicho, wapiganaji wa M23 na wala sio wanajeshi wake ndio waliokuwa
katika eneo ambalo makombora hayo yalirushwa'' Alisema Kanali Hamuli.
Matamshi hayo yaliungwa mkono na msaidizi wa
katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Mulet ambaye aliiambia Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, wanajeshi wake nchini DRC walishuhudia
wapiganaji wa M23, wakirusha makombora wakilenga Rwanda na wala sio
wanajeshi wa Congo.
Takriban watu laki nane wamekimbia makwaoi
nchini Congo tangu waasi hao wa M23 kuanzisha mashambulio katika eneo la
Mashariki mwa Congo Aprili mwaka wa 20120.
BBC