Rafael Nadal bingwa wa wanaume

RAFAEL NADAL Rafael Nadal amemcharaza bingwa wa dunia wa tennis ya wanaume Novak Djokovic kwenye mchuano wa fainali ya shindano la ...


RAFAEL NADAL
Rafael Nadal amemcharaza bingwa wa dunia wa tennis ya wanaume Novak Djokovic kwenye mchuano wa fainali ya shindano la US open mjini New York Marekani na ambalo amelishinda kwa mara ya pili.

Mchuano huo wa seti nne ulikuwa mkali sana.

Nadal raia wa Uhispania na mwenye umri wa miaka 27, alicheza vyema sana na kushinda mchuano kwa 6-2 3-6 6-4 6-1 katika muda wa saa tatu na dakika ishirini na moja.
Nadal sasa ameshinda mashindano 13 makubwa ya Grand Slam na kusemekana kuwa mchezaji pekee anayeweza kumkaribia aliyekuwa bingwa wa tennis Pete Sampras.
Na baada ya kukosa kushiriki michuano ya US Open mwaka jana kutokana na jeraha, Nadal sasa anajiandaa kuchukua nafasi ya kuwa mchezaji nambari moja wa Tennis duniani.
"ushindi wangu umenifurahisha sana,'' alisema Nadal akiongeza kuwa hakutarajia kushinda. ''Hivyo ndivyo maisha yalivyo, na nina bahati sana.''
"napenda sana ushindani na pia napenda sana mchezo huu. Maisha yangu yote nimekuwa nikiota kuhusika na mashindano kama haya.

Related

NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika kwenye Uwanja ...

MAALIM SEIF ATEMBELEA ENEO LA JENGO LILILOANGUKA JANA MJI MKONGWE ZANZIBAR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akimsikiliza Kamanda Ame Ali ambaye ni kiongozi wa shughuli za usafishaji wa eneo lilipoanguka jengo la ghorofa huko Shang...

TAMISEMI YATANGAZA TAREHE YA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Bwn. Khalist Luanda akizungumuza na waandishi habari juu ya kukamilika kwa maandalizi ua uchaguzi wa Serikali za Mitaa miji Dodoma leo. Bwn. Khalist Luanda ...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904755
item