TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyang...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/09/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari.html
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.
Ziara hiyo
itaanzia katika mkoa wa Shinyanga septemba 10 mpaka 13 mwaka huu, kwa
kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa
Simiyu kuanzia Septemba 14 mpaka septemba 19 kwa kutembelea wilaya zote
tano Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea wilaya Sita za mkoa
wa Mara kuanzia Septemba 20 Mpaka 25 mwaka huu.
Katika ziara
hiyo Katibu Mkuu wa CCM ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.
Kwa mujibu wa
Ratiba ya ziara hiyo, Wajumbe hao wa sekretarieti watakagua uhai wa
Chama ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya sanjari na kuhamasisha
wananchi kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika
maisha Yao na ya taifa kwa ujumla.
Aidha watakagua
maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015
hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili
ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye
tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo
Barabara.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu atapata
fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na
serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya
mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
05/09/2013