MIJI YA LINDI NA MTWARA KUSHIRIKIANA NA NORWAY
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mwenye koti refu) akijadiliana jambo na Meya wa mji wa Sandnessjoen, Bard Anders (...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/10/miji-ya-lindi-na-mtwara-kushirikiana-na.html
Waziri
wa nishati na madini, Profesa Sospeter Muhongo na viongozi wa miji
miwili ya Hammerfest na Sandnessjoen iliyoko nchini Norway wamekubaliana
kuanzisha ushirikiano baina ya miji hiyo na ile ya Lindi na Mtwara.
Uamuzi
huo umefikiwa katika mkutano baina ya viongozi wa miji hiyo na ujumbe
wa wizara ya nishati na madini nchini Norway ambapo wamekubaliana
kukutana mwezi ujao kuweka mikakati ya ushirikiano huo.
Katika
makubaliano hayo viongozi kutoka pande zote wamekubaliana kuwa mji wa
Harmmerfest utashirikiana na Lindi na ule wa Sandnessjoen utashirikiana
na Mtwara, ushirikiano ambao unalenga kuzitumia fursa zilizopo
kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza
mara baada ya kufikia makubaliano hayo Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Muhongo amesema ili kuhakikisha mikoa ya kusini inanufaika na
rasilimali zake, serikali imeamua kushirikiana na wadau wa maendeleo ili
kutimiza azma hiyo.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa wavuvi katika mji wa Sandnessjoen amesema
uhusiano mzuri kati ya serikali na makampuni ya mafuta umechangia
kubadilisha historia ya watu wa maeneo hayo ikiwemo kuwawezesha kukua
kichumi na kuwasaidia kupata huduma mbalimbali za kijamii.
Akizungumzia
umuhimu wa makampuni ya mafuta katita mji wa Sandnessjoen Meya wa mji
huo Bard Anders Lango amesema, kwa kiasi kikubwa mapato ya mji huo
yanatokana na mafuta.
Aidha
Lango ameongeza kuwa asilimia Ishirini na mbili ya mapato yanayotokana
na mafuta inatumika kutoa huduma muhimu za kijamii katika sekta za afya
na elimu.
Naye
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Mafuta la BP Olav
Fjellsa amesema moja ya mbinu ambazo zimeliwezesha shirika hilo kujenga
mahusiano mema na jamii ni kuhakikisha yanatoa misaada katika maeneo
husika, kuwekeana mikataba mizuri pamoja na kujihusisha na ununuzi wa
bidhaa za wazawa.
Kuanzishwa
kwa ushirikiano baina ya miji hiyo na mikoa ya kusini kutasaidia
kufungua ukurasa mpya wa mahusiano na hiyvo kuwezesha wananchi kuwa
sehemu ya mafanikio ya kuanzishwa kwa miradi ya umma katika maeneo yao.
Kabla
ya ugunduzi wa gesi na mafuta miji hiyo miwili ilikuwa ikijishughulisha
na uvuvi, kabla ya serikali ya Norway kuamua kuanzisha shughuli za
uchimbaji wa gesi na mafuta baada ya kufikia makubaliano na wananchi wa
maeneo hayo.