JINSI YA KUJIZUIA USIPATE SARATANI YA MATITI (BREAST CANCER)

1. JICHUNGUZE MATITI YAKO. Ukijichunguza mwenyewe mapema inasaidia kugundua saratani mapema na kutibika kwa urahisi, unatakiwa kujic...


1. JICHUNGUZE MATITI YAKO.
Ukijichunguza mwenyewe mapema inasaidia
kugundua saratani mapema na kutibika kwa
urahisi, unatakiwa kujichunguza walau mara
moja kwa mwezi baada ya wiki moja ya
kwanza kupita baada ya hedhi, na wasiopata
hedhi wajichunguze tarehe za mwanzo wa
mwezi, unapo kandamiza ziwa lako kwa
ndani ukihisi kuna uvimbe au nundu(kitu
kingumu) na maumivu,basi fanya mapema
ukamwone daktari kwa uchunguzi zaidi.

2. Mammogram (Hiki ni kifaa chenye uwezo wa
kuonesha uvimbe ndani ya titi)
Wanawake wenye umri zaidi ya miaka 40
wanashauriwa kufanya hiki kipimo walau
mara moja kwa mwaka hata kama kwenye
familia yake hakuja wahi kuwa na tatizo la
saratani ya matiti, wanawake wanashauriwa
kuanza kipimo hiki katika umri wa miaka 30
kama kwenye familia yake dada au mama
yake alikuwa na saratani ya matiti.

3.MAMA KAMA ANA MTOTO ANAYE NYONYA
USIACHE KUMNYONYESHA
Wanawake wengi katika ulimwengu wa
kisasa huacha kunyonyesha watoto maziwa
wakiofia kualibu muonekano wa maumbile
yao, hii ni hatari kwani huongeza hatari ya
kupata saratani ya matiti, uchunguzi
unaonesha kwamba akina mama
wanaonyonyesha watoto wao mpaka umri wa
miaka 2 huzuia hatari ya kupata saratani ya
matiti kwa 60%, sababu ni kwamba
kunyonyesha mtoto hupunguza mizunguko
ya siku za hedhi na hupunguza kiasi cha
estrogen ambayo husababisha kansa

4. KUWA NA UZITO WA KAWAIDA
Wanawake ambao wana maumbo makubwa
yani unene wanapofikia (menopause) ni
kipindi ambacho hawezi kuzaa tena huwa
katika hatari ya kupata saratani ya matiti,
kabla ya kufikia kipindi hichi mirija ya uzazi
ndiyo hutengeneza estrogen na kiasi kidogo
tu hutengenezwa na seli za mwili. Baada ya
menopause, mirija ya uzazi huacha
kutengeneza estrogen hapo sasa estrogen
hutengenezwa na mafuta ya mwili, kuwa na
mafuta mwilini mengi maana yake pia una
estrogen nyingi ambao hupelekea saratani ya
matiti. Kwa afya nzuri mwanamke
anashauriwa kuwa na BMI chini ya 25.

5. KUPIMO CHA MAGONJWA YA KURITHI(GENETIC
TESTS)
Ni pekee 5 hadi 10% ya saratani ya matiti
husababishwa kutoka mabadiliko ya ghafla ya
jene kutokana na kurithishwa jene za kansa
(gene mutations).

6. KUFANYA MAZOEZI
Kufanya mazoezi pia kuna punguza hatari ya
kupata saratani ya matiti fanya mazoezi walau
dakika 30 kwa wiki mara tatu, hii itasaidia
kuunguza mafuta mwilini, kuwa mwepesi na
kuongeza kinga ya mwili. Mazoezi
yanashusha kiwango cha estrogen , na
mazoezi yanapunguza hatari ya saratani ya
matiti kwa 20 hadi 40%, pia unaweza
kufanya mazoezi ya kuongeza pumzi kwa
kutembea haraka.

7. KULA VYAKULA VISIVYO KUWA NA MAFUTA MENGI.
Vyakula visivyo kuwa na mafuta mengi
hupunguza hatari ya saratani ya matiti,
humfanya mtu asi nenepa. Kwani kiasi cha
mafuta mwilini kikiwa kingi huleta saratani ya
matiti.

8. PUNGUZA KIASI CHA POMBE UNACHOKUNYWA
(KI LEVI)
Punguza kiasi cha pombe unachotumia kwani
sumu iliyopo kwenye kilevi huenda moja kwa
moja kushambulia DNA ambapo husababisha
kansa, mwanamke anaye kunywa bia 2 hadi
5 kila siku huzidisha 1.5 ya hatari kupata
saratani ya matiti, ukilinganisha na asiye
kunywa pombe, acha kabisa unywaji wa
pombe ikiwezekana tumia bia 1 tu kwa siku
kwa ajili ya afya.

9. KULA MAHARAGE YA SOYA
Kula maharage soya na viginge vinavyofanana
na soya itapunguza hatari ya saratani ya
maziwa, soya ina mchanganyiko wa
isoflavones hii huungana na seli za mwili na
kuizuia estrogen kutengeneza seli za saratani
ya matiti.

10. USIWE KARIBU NA DAWA ZA KUUA WADUU NA
KEMIKALI ZA AINA YEYOTE.
Usiwe navyo karibu kwani zina tabia kama
estrogen ambazo husababisha seli za saratani
za matiti kujizalisha haraka, pia husababisha
ugonjwa kuenea haraka.

11. PUNGUZA KIASI CHA MIONZI
Wanawake waliofanyiwa matibabu ya mionzi
kwenye kifua kama ugonjwa wa Hodgkin`s
na non-hodgkin`s lymphoma au acne wapo
katika hatari ya kupata saratani ya matiti, kiasi
cha kupata saratani ya matiti kwa mionzi
inategemea na umri, walio na umri ya miaka
zaidi ya 40 wakipata matibabu yoyote yale ya
mionzi hawaongezi hatari ya kupata na
saratani ya matiti.
 
 
  

Related

TUJUZANE 8678284880055598985

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item