RAIS KIKWETE AWAPANDISHA VYEO MAKAMISHNA 77 JESHI LA POLISI

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa 77 wa Jeshi la Polisi kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Ka...

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa 77 wa Jeshi la Polisi kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP). Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Msemaji wa jeshi hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Advera Senso imesema waliopandishwa vyeo ni pamoja na makamanda wa polisi wa mikoa mbalimbali nchini.  
Aliwataja baadhi ya maofisa hao kuwa ni Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo na Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi.
Makamanda wengine waliopandishwa vyeo na mikoa yao kwenye mabano ni Diwani Athumani (Mbeya), Frasser Kashai (Kigoma), Geofrey Kamwela (Singida), Faustine Shilogile (Morogoro), David Misime (Dodoma) na Ferdinand Mtui (Mara).
Wengine ni Costantine Massawe (Tanga), Leonard Paul (Geita),  Ulrich Matei (Pwani), Evarist Mangala (Shinyanga)  Deusedit Nsimeke (Ruvuma), Fulgence Ngonjani (Njombe), George Mwakajinga (Lindi) na Dhahiri Kidavashari (Katavi).
Wengine ni baadhi ya makamanda wa vikosi, wakuu wa vitengo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
Mara ya mwisho kwa maofisa wa jeshi hilo kupandishwa vyeo ilikuwa Mei mwaka kuu wakati makamishna wawili na manaibu kamishna 19 walipoteuliwa.
Miongoni mwa walioteuliwa walikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar e Salaam, Suleiman Kova na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, Isaya Mngulu walipopandishwa cheo kutoka Naibu Kamishna (DCP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP).
Miongoni mwa waliopandishwa vyeo na kuwa manaibu kamishna wa Polisi ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, Thobias Andengenye na Michael Kamuhanda.
Chanzo -  Mwananchi

Related

SAKATA LA KOROSHO LIWALE, NYUMBA 20 ZATEKETEZWA

 Takriban nyumba 20 zimeteketezwa katika maandamano yaliyofanywa na wakulima wa Korosho pamoja na waandamanaji wengine Kusini mwa Tanzania. Hii ni kwa mujibu wa mbunge mmoja wa eneo hilo.Mb...

WANAWAKE KWENYE MIEREKA TUPO, HII NI KUTOKA SENEGAL

Nchini Senegal, miereka ya kitamaduni inapendwa zaidi kuliko soka huku wachezaji wakijipatia pesa nyingi na hata kuwa watu maarufu. Katika sehemu nyingi za nchi mchezo huu ni wa wanaume pekee la...

MBUNGE AMWONYA RAIS KUTOIPIGIA DEBE CCM

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete asiitumie ziara yake ya Mkoa wa Mbeya kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi(CCM) bali afanye kazi za kiserikali. ...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904746
item