TASWIRA MBALIMBALI ZA MAZISHI YA DKT. MVUNGI KIJIJINI CHANJALE MWANGA KILIMANJARO
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha Josephat Lobullu (kulia) na Askofu wa Jimbo la Same Rogath Kimaryo wakiongoza ibada y...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/11/taswira-mbalimbali-za-mazishi-ya-dkt.html
|
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la
Arusha Josephat Lobullu (kulia) na Askofu wa Jimbo la Same Rogath Kimaryo
wakiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Dkt. Sengondo Mvungi. Ibada hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chanjale wilayani
Mwanga mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa pia na Askofu Damian Dallu (katikati) wa
Jimbo la Geita Jumatatu, Novemba 18, 2013. |
|
Mke wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu
Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi akiweka shada la maua katika kaburi la
mume wake wakati wa mazishi. |
|
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi James Mbatia wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi wakati wa mazishi. |
|
Jeneza lenye
mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi
likishushwa kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini Chanjale wilaya
ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013. |
|
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, mkewe Mama Tunu,
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na viongozi
wengine wakifuatilia ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi. |
|
Familia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi ikifuatilia ibada ya mazishi
iliyofanyika katika kijijini cha
Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013. |
|
Askofu Damian Dallu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita akiongoza
ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu
Dkt. Sengondo Mvungi katika makaburi ya familia kijijini Chanjale wilaya ya
Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013 |
Source:
http://mwanawaafrika.blogspot.com