AFRIKA KUSINI WAFANYA IBADA MAALUM YA MANDELA
Johannesburg. Afrika Kusini, jana ilitawaliwa na ibada na maombi yaliyofanyika katika makanisa mbalimbali kuliombea taifa, baada ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/12/afrika-kusini-wafanya-ibada-maalum-ya.html
Johannesburg.
Afrika Kusini, jana ilitawaliwa na ibada na maombi yaliyofanyika katika makanisa mbalimbali kuliombea taifa, baada ya kifo cha Rais wa Kwanza mzalendo, Nelson Mandela.
Afrika Kusini, jana ilitawaliwa na ibada na maombi yaliyofanyika katika makanisa mbalimbali kuliombea taifa, baada ya kifo cha Rais wa Kwanza mzalendo, Nelson Mandela.
Rais Jacob Zuma alikuwa miongoni mwa waumini wa
Kanisa la Bryanston Methodist, Johannesburg katika ibada ambayo pia
ilihudhuriwa na mtalaka wa Mandela, Winnie Madikizela pamoja na mjukuu
mkubwa, Mandla.
Ibada za aina hiyo ziliendeshwa kila kona ya nchi,
zikiwaweka pamoja Waafika Kusini ambao waliitikia wito wa Rais Zuma wa
kuitumia Jumapili kuliombea taifa hilo.
Nyimbo za dini zilisikika katika kumbi za ibada na
makanisa, ambako viongozi wa Serikali wakiwamo Naibu Rais wa Afrika
Kusini, Kgalema Motlante na Rais Mstaafu, Thabo Mbeki walikuwa miongoni
mwa waliopangiwa kushiriki katika ibada hizo.
Katika Kanisa la Baptist, baadhi ya waumini wakiwa
katika mavazi rasmi walionekana wakiimba na kucheza, kabla ya Rais Zuma
kupewa nafasi ya kuzungumza.
“Kwa nchi yetu, kifo cha Baba Madiba ni hasara ya aina yake. Waafrika Kusini tunapaswa kuomba tukikumbuka mambo mema ya kiukombozi na uhuru, amani, msamaha, haki na kujali ambayo Mandela aliyapigania na kuyasimamia,” alisema Zuma.
“Kwa nchi yetu, kifo cha Baba Madiba ni hasara ya aina yake. Waafrika Kusini tunapaswa kuomba tukikumbuka mambo mema ya kiukombozi na uhuru, amani, msamaha, haki na kujali ambayo Mandela aliyapigania na kuyasimamia,” alisema Zuma.
Kwa upande mwingine, mamia ya wafuasi wa Chama cha
African National Congress (ANC), walifurika katika Ukumbi wa Benki ya
Standard, Johannesburg kushiriki katika maombi, wakiitikia wito wa Rais
Zuma.
Mwandishi wetu alishuhudia makada wa chama hicho
wakiwa katika mavazi rasmi, wakicheza muziki wa Injili na baadaye
wakishiriki maombi yaliyowahusisha waumini wa madhehebu ya Kikristo,
Kiislamu, Kihindu, Kiyahudi, Bahai na wale wanaoamini katika imani za
jadi.
Qunu kimya
Wakati nyimbo na ngoma zikichezwa kwa ajili ya
kusifu kazi alizofanya Mandela, katika Kijiji alichokulia Qunu, eneo la
Mthatha kuliripotiwa kuwa kimya huku wakazi wake wakikataa kuzungumza na
waandishi wa habari kuhusu kifo cha Mandela.
Wanakijiji hao wameamua kukaa nyumbani
wakiomboleza na inaaminika kwamba wengi hawaamini kilichotokea na
pengine wanasubiri kushuhudia mwili wa kiongozi huyo utakapofikishwa
huko Jumamosi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumapili.
Hata hivyo, hali ni tofauti katika Kijiji cha Mvezo alikozaliwa
Mandela, ambako tangu Ijumaa, wakazi wake wamekuwa wakiamka asubuhi na
kushiriki katika ibada na maombi hadi adhuhuri, kisha kurejea tena
jioni.
Kitukuu wa Mandela, Mambui alisema hali katika
kijiji hicho kilichopo umbali wa Kilometa 25 tu kutoka Qunu ni ya huzuni
na kwamba watu wake wamekuwa wakiomboleza kwa kulia machozi hasa
wanapokuwa katika nyumba zao.
“Ni machozi ya huzuni na maumivu moyoni, siyo
machozi ya furaha hata kidogo,” alisema Mambui alipokuwa akihojiwa moja
kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Afrika Kusini (SABC), jana
asubuhi.
MWANANCHI
MWANANCHI