MAITI YAKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA MOROGORO

MWILI wa marehemu, Khalid Abdul Kitala (47) ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam ukiwa katika chumba cha kuhifadhi...

MWILI wa marehemu, Khalid Abdul Kitala (47) ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro muda mfupi kabla ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na kete 17 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya katika tukio la kufasarisha maiti iliyotiliwa shaka na askari polisi Mikumi ambao waliweka mtego kufuatia kupata taarifa za tukio hilo na raia wema na kulinasa gari lililokuwa likitokea Iringa kwenda Dar es Salaam majira ya saa 21:26: HRS jana usiku.

Maiti ikiwa ndani ya gari aina ya SPACIAL yenye namba ya usajili T 887 BSW eneo la nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro, baada ya gari hilo kukamatwa majira ya saa 7 usiku eneo la Mikumi, likiwa na watu watatu na maiti ya binadamu inayodaiwa kupoteza maisha baada ya kumeza kete  zinazohisiwa kuwa ni madawa ya kulevya na kufariki dunia, ikisafirishwa kutoka Tunduma mkoani Mbeya kwenda Jijijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa wa tukio hilo

Polisi wakikagua gari hilo


HIZI ndizo kete zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya yaliyopatikana katika gari baada ya kupekuliwa kituo kikuu cha polisi.

Polisi mjini Morogoro imewakamata watu watatu wakiwa na maiti iliyobebeshwa kete 17 zinazoaminika ni dawa za kulevya, Katika gari la watuhumiwa lilipekuliwa kwa kina na kupatikana kete 7 na kete 17 na kufanya jumla yake kuwa 24 zilizokamatwa na watuhumiwa wapo chini ya ulinzi katika kituo kikuu cha polisi kwa uchunguzi;  uchunguzi unaendelea.

Picture Credit: Mtanda Blog

Related

OTHER NEWS 7805528200442351845

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item