TAMKO LA WANACHADEMA WA MKOA WA MWANZA HILI HAPA
Ndugu wanahabari, muda mfupi uliopita (jana) tumetoka kufanya mkutano na waandishi wa habari hapa mwanza kwenye ukumbi wa HILL FRONT ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/12/tamko-la-wanachadema-wa-mkoa-wa-mwanza.html
Ndugu wanahabari, muda mfupi uliopita (jana) tumetoka kufanya mkutano na
waandishi wa habari hapa mwanza kwenye ukumbi wa HILL FRONT sisi kama
wanachama wa chadema kuelezea msimamo wetu dhidi ya kinachoendelea hivi
sasa ndani ya chama.nimeweka kopi ya taarifa yetu na kui attach pia.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI
Ndugu
wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi wa matawi 189 ya
chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa mwanza. Umoja huu wa matawi
unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.
Hivyo
katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30.nov 2013 kuanzia saa nne
asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia
kuanzisha umoja huu wa wanachama.
Hii
ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wetu wanaotuwakilisha kwenye
vikao vya maamuzi kama vile wilaya, mkoa na taifa wamekuwa waoga na
wameshindwa kuwakilisha mawazo yetu tuliyowatuma badala yake wengi wao
wamekubali kuwa vibaraka wa kile kinachoitwa CHADEMA KASKAZ
Kutokana
na ukweli kwamba msingi wa chama chetu na chama kingine chochote kile
cha siasa, uimara na uhai wake unatokana na uwepo wa misingi na matawi
ya chama, hivyo sisi wanachama wa matawi haya 189 tumeamua kuunganisha
nguvu zetu kutetea chama chetu na kuhakikisha haki, heshima, katiba na
maadili ya chama vinafuatwa bila ya kuogopana wala kuoneana haya.
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
Chadema
ni chama cha siasa kinachopaswa kuendeshwa kwa misingi ya kufuata
taratibu, kanuni na katiba yake na si vinginevyo. Lakini badala yake
kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa juu kujitwalia
mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama chetu hususan
katika kutoa haki sawa kwa viongozi na wanachama wa chama chetu.
Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya juu sana kwa wale wanao amini kuwa
ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo kupelekea kuwaadhibu kama ndio
kinga yao ya kuendelea kuongoza bila kuhojiwa au kukosolewa.
Sababu zilizotolewa na kamati kuu hazikubaliki
Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe 20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi Kabwe, Dr. Kitila Mkumbona Ndg Samson Mwigamba,
kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali ni unafki na Uzandiki
wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa Demokrasia kwa
kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama. Katiba yetu imeweka
wazi Ibara ya 6 Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za
nidhamu na uwajibishaji ndani ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya
kufanya maamuzi bila kufuata taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo
sisi baadhi ya wanachama huo ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi
ndani ya chama kwa viongozi wetu waliotumia nguvu zao na akili nyingi
sana kukijenga chama.
Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni
1. Kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za serikali.
2. Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
3. Harambee za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
4. Kutaka
kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana
wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki
ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
5. Kutaka
kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote
kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao
makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.
Kushamiri kwa migogoro
Mwenyekiti
na katibu mkuu wameshindwa kutatua migogoro ya viongozi na wanachama
kutoka mikoani kwa njia sahihi za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya
kwa viongozi na wanachama kutumia njia ya mitandao ya kijamii
tukiongozwa na katibu mkuu mwenyewe, kujitokeza mara kwa mara kwenye
mitandao hiyo hiyo kwa madai ya kutolea ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya
husuyo maswala ya chama ilihali akijua kufanya hivyo ni usaliti mkubwa
kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao ilipelekea migogoro mikubwa
sana hususan mkoa wetu wa Mwanza na kupelekea kupoteza Halmashauri ya
Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa
uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya chama na kutumia nafasi zao
kuopanga safu za uongozi wanao uwona watawatumikia wao na si chama,
hivyo kusababisha mifarakano mikubwa ndani ya chama na kupelekea
kuvuliwa uongozi kwa viongozi mbalimbali katika mkoa wetu kwa maamuzi
yasiyo zingatia utafiti na uhalisia wa kweli ndani ya chama.
Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja katiba Mfano:
Hitimisho
ROBERT E. GWANCHELE
· Kitendo
cha kutoa muongozo nje na matakwa ya katiba juu ya kuwapata wawakilishi
kwenye vyombo vya maamuzi kama wabunge kwamba wanaohitaji kugombea 2015
waandike barua makao makuu na wao ndio watatoa wagombea kinyume na
katiba ya chama Ibara 7.2.13 inayotoa taratibu ya kuwapata wagombea,
huwo ni uvunjaji wa katiba na ubakaji wa demekrasia ndani ya chama,
sizani kama kuna uhaini zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama
leo sisi Chadema hatuheshimu katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe
itakuwaje siku tukikabidhiwa nchi yenye watu wenye mawazo na mtizamo
tofauti na sisi?. Hatutaki kuamini kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja
wa maopambano ya kivita.
Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lema kumkashfu kiongozi wa chama Mh: Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na Mzandiki kwendye mitandao ya kijamii pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw Henry Kilewo kwa
kuweka waraka unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu Zitto mbao chama
makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama kukana
mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo chama hakiusiki nao na
hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw Kilewo ambaye pia ni
kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama, waraka huo ambao
chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali akijua kufanya
hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu maadili ya
viongozi kanuni ya 10.
Pia
tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa kwa waandaaji wa tamthilia
hii ijulikanayo kama Ripoti ya siri kuhusu Zitto kwasababu tayari makada
na viongozi wetu wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni mwa waandaaji wa
tamthilia hii.
Lakini
cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia macho na kupelekea kwetu baadhi ya
wanachama kuamini zengwe hili la kumchafua Zitto Lina Baraka zote za
viongozi wa chama ngazi ya juu.
Tunataka
kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa
waraka ujulikanao kama mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo
itumike kwa hawa waliotumia njia chafu ya kuandaa waraka wa kumchafua
zitto ambao chama kinawajua na baadhi yao tumewaweka humu kwenye tamko
letu.
Kingine
tunataka kwa mara nyingine kwa viongozi wa chama makao makuu kuwaambia
umma wa watanzania ni kwanini waraka huo huo uinaoitwa warajka wa siri
kuhusu Zitto leo viongozi na wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka
huo uangawiwa kwa wanachama na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si
ubaguzi ni nini?.
Tunaonya
na kulaani kitendo cha viongozi wetu kuendeleza utawala wa kibabe na
kupelekea kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanachama na viongozi
wanaotofautiana nao kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya baadhi ya
viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja
jukwaani hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia maneno ya uchochezi dhidi
ya wanachama na viongozi wanaokinzana nao kifikra na kimtizamo na
kuhamasisha wanachama wasiojua itikadi vizuri ya chama kuwa
wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa hadharani kwenye
mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli kubaki na
maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali kuhusiana na
jambo hili.
Hitimisho
Mwekiti
na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na
matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan
chi hii, M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba
kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza
uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa
Demokrasia.
Mwisho
tunataka maamuzi haya HARAMU kamati kuu yabatilishwe na mchakato wa
kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni kwa mujibu
wa katiba tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na wapigania
Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka
uongozi uliopo utoke madarakani.
Vile
vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote
wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na
highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya
ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo
tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.
Tunamuagiza
mbowe na slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa
bado hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu,tumekuwa
wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama
hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha, Sasa
sisi wanachadema wa matawi ya mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla,
tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi watupo chadema kwa bahati
mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi wakuu wa chama hiki,
tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob Nyanga Makani,
Marehemu Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, kamanda Zitto
Kabwe na sisi wengine wengi.
Vyovyote
itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu
unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA
ROBERT E. GWANCHELE
Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA
0757 084776