ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE AZIDI KUPEWA MISAADA.

WADAU mbali mbali na wasamaria wema wamezidi kujitokeza kumpa msaada wa hali na Mali,Aida Nakawala(25) mkazi wa kijij...








WADAU mbali mbali na wasamaria wema wamezidi kujitokeza kumpa msaada wa hali na Mali,Aida Nakawala(25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, aliyejifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadruplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya.
 
Misaada hiyo imeongozana ikiwa ni siku moja baada ya Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Vanesa pamoja na Mbeya yetu kutoa misaada mbali mbali ambapo jana Kampuni ya Arif Electronic nayo imeguswa.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo pamoja na familia yake, Faizar Kasamia, baada ya kuguswa na hali ya Mama huyo ametoa vitu vya aina mbali mbali vyenye thamani ya Shilingi Laki tatu.
Vitu alivyotoa ni pamoja na Nguo, Maziwa (Lactogen), Mafuta, Sabuni na Nepi.

  Na Mbeya yetu

Related

OTHER NEWS 9151172459408955083

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item